Alhamisi 25 Septemba 2025 - 13:40
Uhispania yaionya Israel kuhusu kuzilenga meli zinazobeba misaada kwa ajili ya watu wa Ghaza

Hawza/ Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania, José Manuel Albares, katika tamko lake la hivi karibuni aliionya Israel kuwa shambulio lolote dhidi ya meli Samoud Fololita ambayo inabeba misaada ya kibinadamu kuwapelekea watu wa Ghaza, litakabiliwa na majibu makali.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza, katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uhispania imeelezwa kuwa tishio au shambulio lolote dhidi ya meli inayobeba misaada ya kibinadamu kwa watu wa Ghaza litafuatiliwa na kukabiliwa kwa majibu makali.

Amesisitiza juu ya asili ya amani na ya kibinadamu ya jukumu la meli hii na akaongeza kuwa Madrid inatoa ulinzi wa kibalozi kwa raia wote wa Kihispania walioko ndani ya meli hiyo. Hatua yoyote dhidi ya abiria waliopo kwenye meli ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa katika maji ya wazi na ni uvunjaji wa sheria za kimataifa za Umoja wa Mataifa, na itashughulikiwa kwa ukali.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania vilevile alimwita mwakilishi wa Tunisia nchini humo ili ampe jukumu la kuchunguza kuhusiana na shambulio la ndege zisizo na rubani dhidi ya msafara wa misaada ya kibinadamu unaoelekea Ghaza.

Chanzo: MEM

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha