Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, vyanzo vya habari vimeripoti kuhusu kuongezeka kwa operesheni za kuhamisha watu kwa mfumo maalumu inazofanywa na magenge ya al-Jaulani, ambayo yanalenga koo mbalimbali mjini Damaski, mji mkuu wa Syria.
Vyanzo hivyo katika mazungumzo yao vilisema: Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, tumeshuhudia kushambuliwa kwa mitaa tisa ya makazi yaliyopo mashariki, kusini na kaskazini mwa Damaski, mji mkuu wa Syria, kwa lengo la kuhamisha koo, hususan koo ya Alawi, kwa njia ya kuwateka nyara wanachama au kwa njia ya vitisho na mashambulizi kwa kutumia vifaa vya sauti na milipuko, sambamba na kushambulia makaburi ya mashahidi na maeneo ya kidini.
Vyanzo hivyo vimeongeza kuripoti kuwa: Mamia ya familia, zinazokabiliwa na shinikizo la hatua hizi, wamelazimika kuacha makazi yao kama sehemu ya mabadiliko ya kimfumo wa nguvu yanayofanywa waziwazi na magenge hayo.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mashambulizi haya hayakujikita kwa koo ya Alawi pekee, bali yaliwahusu pia Wakristo, huku kukiwa na makumi ya nyaraka zinazothibitisha uwepo wa jitihada kubwa za kubadilisha sura na tabia za mitaa ambayo kwa miongo mingi imetambulika kwa mshikamano wa amani na mwingiliano wa kijamii, hususan katika maeneo ya kale.
Ni jambo la kutilia maanani kuwa magenge ya al-Jaulani yana historia nyeusi ya uvunjaji wa haki za binadamu na mauaji ya kimbari dhidi ya jamii za Kisyria katika miezi ya karibuni.
Maoni yako