Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanchi, Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba za Swala ya Ijumaa alizozitoa katika Husayniyya Azam Fatimiyya Najaf Ashraf, alisema: Shambulizi la Israeli dhidi ya Doha na mabomu yaliyorushwa Yemen yamekabiliwa na ukimya wa dunia, isipokuwa baadhi ya matamko ya kulaani ya aibu hapa na pale, tunayo haki ya kudai adhabu dhidi ya Israeli kutokana na jinai hizi, na Umoja wa Mataifa umeyalaani makosa haya.
Katika sehemu nyingine ya khutba zake alieleza: Wiki hii, mkono wa kulia wa Trump ameuawa kwa shambulio, na Marekani imetangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa kwa sababu ya tukio hili, tukio kama hili lilitokea mara ya mwisho mwaka 1963 wakati wa kuuawa kwa Kennedy, rais wa Marekani.
Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf akaongeza kusema: Hii inamaanisha kuwa mazingira ya Marekani hayana usalama, bali kuna mgogoro wa ndani wa kweli ndani ya Marekani.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanchi alisema: Suala la Palestina limekuwa suala la kimataifa, walitaka kulisahaulisha kihistoria, lakini limegeuka kuwa suala hai linalosababisha mpasuko ndani ya nyumba ya Kiyahudi.
Kuhusiana na uamuzi wa Bunge la Marekani alisema: Uamuzi wa Bunge la Marekani wa kufuta haki ya rais kutangaza vita dhidi ya Iraq ni msimamo ulio katika njia sahihi.
Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf akiendelea kuhusu baadhi ya matamko ya kimadhehebu yanayodai mauaji ya kimbari na kufukuzwa kwa Mashia, alisema: Tuwajibu vipi wanaosema haya? Maimamu wetu wametufundisha tusijibu matusi kwa matusi, wala laana kwa laana, bali tuwajibu kwa wema, kwa lugha ya Qur’ani ambayo ni msamaha, na tupanue vifua vyetu kwa wote;
«وَیَدْرَؤُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ»(Nao hujibu ubaya kwa wema).
Khatibu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf katika khutba ya kidini kwa mnasaba wa kuzaliwa kwa Imamu Ja‘far al-Sadiq (a.s.) alieleza maana ya neno “Ja‘fari” hivi: Katika hadithi tukufu kutoka kwa Imamu al-Sadiq (a.s.) imesemwa: “Iwapo mtu miongoni mwenu atakuwa mchamungu katika dini yake, mkweli, mwaminifu na mwenye tabia njema, atasemekana kuwa yeye ni Ja‘fari.”
Akasema kwa kusisitiza: Leo hii, kupitia tabia zetu njema, elimu ya Ahlul-Bayt (a.s.), na kupitia jihadi, kujitolea na kuutetea Uislamu na Waislamu kwa bendera ya ulinzi mliyoibeba na mnaopigana kwa ajili yake, sisi ndio wawakilishi wa akhlaqi ya kweli ya Ja‘fari ambayo Imamu al-Sadiq (a.s.) ameashiria katika hadithi yake.
Maoni yako