Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, sherehe za Wiki ya Umoja zinaandaliwa kwa uratibu wa Kituo cha Harakati ya Kiislamu Nigeria, na kwa kuwaalika wa wahadhiri wa kidini wa ngazi ya juu, katika miji mbalimbali ya Nigeria, shughuli hizi zinafanyika chini ya usimamizi wa Ayatollah Ibrahim Zakzaky na zilianza tarehe 12 Rabiul-Awwal.
Miongoni mwa mfululizo wa vikao hivi, katika hafla iliyofanyika siku ya Jumapili jijini Abuja, Sheikh Haliru Maraya — mmoja wa walimu na wanazuoni wa Kiislamu — katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa mshikamano na umoja wa umma wa Kiislamu, na akakumbusha ulazima wa jambo hilo.
Sherehe hizi zimeendelea hadi tarehe 17 Rabiul-Awwal.
Chanzo: Tovuti rasmi ya Harakati ya Kiislamu Nigeria
Maoni yako