Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Mudarrisī amesisitiza kuwa jinai za Wazayuni dhidi ya raia Waislamu zinaonyesha uhalisi wa wanyama na ukatili wao.
Akaashiria pia kuwa hawa hata kidogo hawana huruma au upendo wa wanyama, jambo linalotokana na mitazamo yao ya ubaguzi wa rangi na misingi yao ya kiburi, wanayoiona kila binadamu kama yupo chini ya hadhi yao.
Ayatullah Mudarrisī katika somo lake la maadili la kila wiki kwa wanafunzi na wanazuoni wa Hawza ya Karbala, alibainisha kuwa mojawapo ya sifa muhimu za mwanafunzi wa kweli wa dini ni kuwa na ufahamu wa wakati na jitihada za kusaidia wanyonge.
Huyu mwanazuoni wa Iraq, akibainisha hali mbaya ilivyo katika nchi za Kiislamu na umuhimu wa kujiandaa mara moja dhidi ya uvamizi wowote wa maadui wenye kiburi ambao wanapora rasilimali, fedha, maamuzi na hata silaha na vifaa vya wananchi, alifafanua kuwa maandalizi haya yanapaswa kufanywa sio wakati wa vita au janga, bali muda mrefu kabla yake.
Akaashiria aya moja kutoka katika Qur’ani Tukufu inayosema:
"Na ingeli kuwa kweli walitaka kutoka bila ya shaka wangeli jiandalia maandalio, lakini Mwenyezi Mungu kachukia kutoka kwao, na kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanao kaa."
(Surat Tawba: 47)
Ayatullah Madrasī, akisisitiza hatari ya kutojiandaa kiakida, kitamaduni, kitaalamu au kifikra, alisema: Jukumu letu ni kujiandaa kwa ajili ya kukabiliana na maadui wa dhulma.
Alisisitiza kuwa chombo muhimu zaidi cha kukabiliana na maovu ni "kuamuru mema na kukataza mabaya", na kwamba mbinu zake hubadilika kulingana na wakati na vyombo vya mawasiliano vinavyopatikana kati ya watu.
Maoni yako