Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika sehemu ya hotuba yake, alipokuwa akiashiria wingi wa jinai na maafa ya kushangaza yanayofanywa na utawala wa Kizayuni uliolaaniwa, ambao unatangazwa na wao wenyewe bila ya aibu na haya, alisisitiza kwa kusema: Japokuwa jinai hizi zinatendwa huku zikiwa zinaungwa mkono wa nguvu na nchi kama Marekani, lakini njia ya kukabiliana na hali hii haijafungwa, na nchi zinazopinga, hususan nchi za Kiislamu, lazima zikate kabisa uhusiano wa kibiashara na hata uhusiano wa kisiasa na utawala wa Kizayuni na kuufanya uwe katika hali ya upweke.
Ayatullah Khamenei aliuita utawala wa Kizayuni kuwa ni utawala ulio katika upweke zaidi na unaochukiwa zaidi ulimwenguni, na akaongeza kwa kusena: Moja ya mistari mikuu ya diplomasia yetu pia inapaswa kuwa, ni kuzihimiza serikali zikate uhusiano wa kibiashara na kisiasa na utawala huu ukiojaa uhalifu.
Maoni yako