Jumatatu 8 Septemba 2025 - 14:40
Wasomaji wa Qur'ani wa Kiirani wang'ara katika Kongamano la Arobaini na Mbili la Kimataifa la Maulidi ya Mtume (S.A.W) huko Lahore, Pakistan

Hawza/ Kongamank la 42 la Kimataifa la Maulidi ya Mtume (saw) limefanyika katika ukumbi wa Iqbal mjini Lahore, Pakistan, kwa ushiriki mkubwa wa wanazuoni, wasomi na wapenzi wa Mtume wa Rehema, na kuunda mazingira yaliyojaa hali ya kiroho, mshikamano na nuru.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuna ya Shirika la Habari la Hawza, Kongamano la 42 la Kimataifa la Maulidi ya Mtume (saw), kwa ubunifu wa taasisi ya Minhaj-ul-Quran International, limefanyika katika Ukumbi wa Iqbal mjini Lahore, Pakistan. Mkusanyiko huu mkubwa ulihudhuriwa na idadi kubwa ya wanazuoni na wasomi mashuhuri, masheikh, q'arii wa kimataifa, waimbaji wa qasida za kidini, pamoja na maelfu ya wapenzi wa Mtume Mtukufu (saw). Tukio hili lilihesabiwa kuwa miongoni mwa matukio ya kudumu, likiwa taswira ya mapenzi na utiifu kwa Mtume Mkuu (saw) na chombo cha kueneza ujumbe wa sira yake katika ulimwengu wa Kiislamu.

Hafla ilianza kwa kisomo cha aya za Qur’ani Tukufu zilichosomwa na qarii wa kimataifa, na hapo ikatawala hali ya kiroho na ya kimaanawi katika mkutano huo, baadaye vikundi vya nashidi kutoka nchi mbalimbali viliwasilisha kasida zilizojawa na mapenzi na utiifu kwenye hadhara ya Mtume Mtukufu (saw), na kujaza ukumbi kwa shauku na hali ya kiroho. Uwasilishaji wa watoto wa Tahfiz-ul-Qur’an pia ulipokelewa kwa mwitikio mkubwa wa hadhira na kuleta nyakati za msisimko na zenye athari.

Katika sehemu kuu ya ratiba, Shaykh al-Islam Dkt. Muhammad Tahir al-Qadri, mwanzilishi na kiongozi mkuu wa Minhaj-ul-Quran, katika hotuba yake, akibainisha nafasi tukufu ya Mtume Mtukufu (saw) ndani ya Qur’ani Tukufu, alisema: Mwenyezi Mungu Mtukufu amemtaja Muhammad (saw) kuwa ni “Taa yenye kung’aa (Siraj Munir)”. Maisha yake yenye nuru ni taa ya uongofu kwa wanadamu wote na ni kielelezo cha kudumu kwa maadili, huruma, rehema na heshima, Mtume wa Uislamu alikuwa ndiye mwenye huruma zaidi, mkarimu zaidi, mvumilivu zaidi na msamehevu zaidi katika historia ya wanadamu.

Akaendelea kwa kusema: Mtume wa Uislamu ana miladi mbili, Miladi ya kimwili ilikuwa katika tarehe 12 Rabi‘ul-Awwal (kwa mujibu wa riwaya ya Ahlus-Sunna), ambayo ilikuwa taswira ya uzuri wa sura yake; na miladi ya kiroho ilikuwa katika wakati wa kutumwa kwa ujumbe (bi‘tha), ambapo nuru ya ukamilifu wake ilikumba ulimwengu wote.

Dkt. Tahir al-Qadri, akieleza juu ya jitihada za baadhi ya harakati katika Bara Hindi kutenganisha baina ya maudhui ya maulidi na sira, alisema: Minhaj-ul-Quran imeziweka mbili hizi pamoja, na leo, mkutano huu wenye haiba unaonyesha kuwa wafuasi wa maulidi na sira wamekusanyika katika safu moja kwa mhimili wa Mtume Mtukufu (saw), wakihamishia mapenzi na ujumbe wake kwa walimwengu.

Mwisho wa hotuba yake, alibainisha kwamba risala ya Mtume wa Uislamu (S.A.W.W) ni risala ya ulimwengu mzima na ya kijumla. Akaongeza: Mitume wote wa Mwenyezi Mungu walitumwa kwa ajili ya kuongoza mataifa yao, lakini Muhammad (saw) ni rehema kwa walimwengu wote na Mtume kwa manabii wote, aliongeza kusema: Katika ulimwengu mzima hakuna sura iliyo na uzuri na ukamilifu kama sura ya Muhammad (saw), na hakuna sira iliyo na usafi na ukubwa kama sira ya Muhammad (saw); kwa kuwa yeye ndiye kielelezo kamilifu zaidi kwa ubinadamu na taa ya uongofu kwa zama zote.

Inafaa kuelezwa kuwa katika hafla hii, qarii mashuhuri wa kimataifa kutoka Iran, wakiwemo Hamed Shakernejad, Ahmad Abolghasemi, na Saleh Mahdizadeh, walihudhuria na kwa kisomo chao cha kuvutia wakaongeza uzuri na mvuto katika ratiba hiyo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha