Ijumaa 5 Septemba 2025 - 18:18
Rais wa Kituo cha Utafiti cha Bunge: Mikakati ya pamoja ya Yemen imedhoofisha biashara ya baharini ya utawala wa Kizayuni

Hawza/ Babak Negahdari alibainisha kuwa hatua za Yemen si tu zimeongeza gharama za utawala wa Kizayuni na Marekani katika eneo, bali pia zimeutikisa ubeberu kwenye sekta ya kiuchumi hasa Marekani, na mizani ya biashara katika Bahari ya Shamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa  Shirika la Habari la Hawza, mjini Tehran, Dkt. Babak Negahdari, Rais wa Kituo cha Utafiti cha Bunge la Kiislamu la Iran, siku ya Alhamisi katika hafla ya kuheshimu juhudi za viongozi wa Yemen iliyofanyika mjini Tehran, alielezea mkakati wa Yemen katika uwanja wa muqawama kuwa wa mshikamano na akasema: “Mkakati huu unaonyesha umoja katika uwanja wa mapambano na umepiga pigo kubwa dhidi ya utawala wa Kizayuni.”

Akiashiria mafanikio ya Yemen katika kulenga biashara ya baharini ya utawala wa Kizayuni, aliongeza kuwa: “Makampuni makubwa ya kizamani ya Magharibi na Kiyahudi yamelazimika kuacha njia hii, hali ya kuwa asilimia 98 ya biashara ya utawala wa Kizayuni hupitia baharini.”

Negahdari alisisitiza: “Hatua za kijeshi za Yemen katika Bahari ya Shamu na Bab al-Mandab zimeleta changamoto kubwa za kijiografia na kiuchumi kwa Tel Aviv, na hata zimeisogeza Bandari ya Eilat hadi kwenye ukingo wa kufilisika.”

Akaendelea kwa kusena: “Licha ya juhudi za Marekani za kujaribu kununua msimamo wa Ansarullah, Wayaemeni wamekataa mapendekezo yote ya kisiasa na kiuchumi na wamesimama imara kwenye muqawama.”

Rais wa Kituo cha Utafiti cha Bunge, huku akieleza kuwa kushindwa kwa utawala wa Kizayuni kunazidi kila siku, alisema: “Mashambulizi ya kiholela ya utawala huu dhidi ya miundombinu na mauaji ya kigaidi ya viongozi wa Yemen yanaonyesha kukata tamaa kwao, na sasa uwanja wa mapambano upo mikononi mwa Yemen.”

Negahdari pia alisisitiza umuhimu wa kuimarisha diplomasia ya bunge na kikanda na akaongeza kusena: “Usafiri salama katika Bahari ya Shamu unapaswa kudumishwa kwa nchi zote, lakini hali ya kutokuwa salama lazima iendelee kwa utawala wa Kizayuni. Yemen inaweza kuelekea kwenye miungano ya kiuchumi na China na Urusi.”

Akiashiria ongezeko la uhalali wa Ansarullah ndani ya Yemen na mwamko wa fikra za umma dhidi ya ujeuri wa Marekani na Uingereza, alisema: “Mafanikio ya Yemen yamevuka mipaka ya nchi hii na Ansarullah sasa imekuwa mchezaji muhimu katika Asia ya Magharibi.”

Mwisho, Rais wa Kituo cha Utafiti cha Bunge alibainisha: “Hatua za Yemen si tu zimeongeza gharama kwenye utawala wa Kizayuni na Marekani katika eneo, bali pia zimeutikisa ubeberu wa kiuchumi wa Marekani na mizani ya biashara katika Bahari ya Shamu, leo Ansarullah ya Yemen imeweza kupiga pigo kubwa katika mishipa ya kiuchumi ya Tel Aviv na malengo yake ya kimkakati.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha