Jumatatu 1 Septemba 2025 - 12:51
Maimamu wa Kiislamu duniani wametaka kuundwa umoja wa Kiislamu kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wa Ghaza

Hawza/ Mkutano wa “Wajibu wa Kiislamu na Kibinadamu; Ghaza” kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni wa Kiislamu na Taasisi ya Wanazuoni wa Kiislamu ya Uturuki na kwa kuhudhuriwa na wanazuoni wa Kiislamu 150 kutoka nchi 50, umehitimishwa katika Msikiti wa Aya Sofia Kubwa

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya  Shirika la Habari la Hawza, Mkuu wa Taasisi ya Masuala ya Kidini ya Uturuki (Diyanet), Ali Erbaş, baada ya Swala ya Ijumaa mbele ya Msikiti wa Aya Sofia, alitangaza kuhusu kufanyika kwa mkutano mkubwa mjini Istanbul kwa ajili ya kuchunguza hatua zinazohitajika kuhusiana na Gaza.

Shughuli hii ambayo ilifanyika kuanzia tarehe 31 Mordad hadi 7 Shahrivar, na ndani yake zikafanyika warsha zikiwa na mada mbalimbali, iliisha kwa kusaliwa Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Aya Sofia.

Erbaş, huku akikumbusha kwamba mkutano ulianza baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Eyüp Sultan kwa kikao cha waandishi wa habari, akizungumzia uhalifu wa utawala wa Kizayuni huko Ghaza alisema: “Baadhi ya serikali duniani zinaonekana zinawasaidia Wazayunu wauaji na watekaji wa watoto na wanawake,” Akaongeza: “Kundi dogo lakini jeuri na lililopotoka, linaipeleka dunia kuelekea janga kubwa, mbele ya dhulma hii ya kutisha na uvamizi usio wa kibinadamu, watu jasiri na wenye heshima wa Palestina hawana chochote zaidi ya imani na nyoyo zilizojaa yakini, nao wanapinga kwa nguvu zao zote, kuunga mkono mapambano halisi ya taifa la Palestina na jitihada za kusimamisha mauaji ya kizazi, bila kujali dini, rangi, madhehebu na utamaduni, ni suala la dhamira na maadili kwa wanadamu wote.”

Erbaş akaongeza: “Kwa kila Muislamu, Ghaza ni suala la imani na uja, katika imani yetu, kutojali mbele ya dhulma na kukaa kimya mbele ya madhalimu, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja ni ushirikiano na wavamizi na wauaji na ni kuwasaidia wao, jambo hili ni haramu na limezuiwa. Hivyo kila mmoja anatakiwa kupaza sauti kwa kadri awezavyo, katika ngazi ya kitaifa na kimataifa, tunapaswa kuendelea na kususia bidhaa za wavamizi wa Kizayuni.”

Mkuu wa Taasisi ya Wanazuoni wa Kiislamu, Profesa Dkt. Nasrullah Hacı Muftüoğlu pia alisoma tamko la mwisho la mkutano.

Akiashiria mauaji yanayoendelea bila kukoma huko Ghaza, ukiukaji mpana dhidi ya mwanadamu na mambo matukufu, ukimya wa kimataifa hasa Marekani na ushirikiano wa baadhi ya pande za kikanda ndani ya mradi wa “Israeli Kubwa”, alisema: “Mkutano wa Istanbul ulifanyika kukabiliana na hali hii.”

Akaongeza: “Mkutano ulifanyika kwa madhumuni ya kutekeleza wajibu wa kidini na kibinadamu katika kusaidia na kuiunga mkono Ghaza na kupitia kikao hiki, wito ulitolewa wa kusimamisha mara moja mashambulizi na kufungua njia za misaada ya kibinadamu.”

Kwa mujibu wake, katika mkutano huu kuliangaziwa umuhimu wa kuunda umoja wa Kiislamu-kibinadamu kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu wa mauaji ya kizazi na kuzuia upanuzi wa Kizayuni.

Tamko la mwisho la mpango huu ambalo lilisomwa na Hacı Muftüoğlu baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Aya Sofia, lilikuwa na vifungu vya kuwaunga mkono watu wa Palestina na kulaani uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni, katika tamko hilo alisema:

“Tunathibitisha kwa yakini kwamba; taifa la Palestina pamoja na mapambano ya kijeshi, lina haki ya kutumia njia zote halali kupambana na uvamizi wa Kizayuni, pia tunaamini kwamba kuhamasisha Umma wa Kiislamu katika aina zote za Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni jambo la lazima kwa ajili ya kuondosha kuzingirwa kwao aridhini, angani na wa baharini huko Ghaza, tunataka hatua za haraka na za kithabiti zichukuliwe, kufunguliwa kwa njia zote za mipaka na nchi jirani ni wajibu, katika muktadha huu, inatarajiwa kwamba msafara wa uhuru uandamane na meli zaidi, tunazishukuru jitihada zote za dhati katika kutetea kadhia ya Palestina na tunatangaza uungaji mkono wetu kamili kwa jitihada za wananchi na hatua rasmi za kusimama pamoja na ndugu zetu wa Ghaza.”

Zaidi ya hapo, tamko hilo liliashiria kwamba wanazuoni waliokuwepo waliwataka Waislamu wote wenye uwezo wa kuunda mfuko wa waqfu na kuhamasisha taasisi zao za kiuchumi na kifedha kwa ajili ya kuunga mkono; na pia angalau asilimia mbili ya faida ya mwaka ipelekwe kusaidia na kuiendeleza Ghaza na hatua hii ifanywe bila kuchelewa.

Akasema: “Mchakato huu lazima ufuatiliwe kupitia mifumo ya kisheria na yenye uwazi ili kuweka msingi wa uungaji mkono wa kudumu kwa ajili ya kuimarisha upinzani wa jamii ya Palestina na maisha yao, Vilevile, ujenzi upya wa Ghaza na kurejesha utulivu na ustawi katika eneo hili, ni jukumu la kibinadamu na faradhi ya kidini mabegani mwa Waislamu wote, hasa wafanyabiashara Waislamu.”

Katika tamko hilo pia ilitakiwa serikali zote, hasa nchi za Kiislamu, zikate mara moja na kikamilifu mahusiano yote na utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake, iwe ya kisiasa, kiuchumi au kijeshi.

“Kununua bidhaa za kampuni ambazo moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja zinashirikiana na Uzayuni, kisheria ni haramu, vilevile kususia njia zote zinazosaidia uvamizi na dhulma ni wajibu, tunatangaza wazi hukumu hii kwa Waislamu wote, viongozi wao na taasisi zao, fatwa hii imejengwa juu ya misingi ya fiqhi ya Kiislamu, makubaliano ya kusaidia waliodhulumiwa na kuzuia madhalimu na inaleta jukumu la lazima kwa Umma.”

Ni lazima maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki na Mahakama ya Jinai ya Kimataifa yatekelezwe na wahusika wa mauaji ya kizazi, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu huko Ghaza wafikishwe mara moja mahakamani, Serikali na taasisi za haki za binadamu pia zinapaswa kuunga mkono mchakato huu kwa ajili ya kutekeleza haki, kurejesha haki za wahanga na kuzuia kurudiwa kwa ukiukaji, kadhalika, nchi za Kiislamu na serikali zote huru zinapaswa kuunda mahakama katika nchi zao kwa ajili ya kuwashtaki wahalifu wa kivita, tunaziomba taasisi za kidini zisizo za Kiislamu, hasa Papa, Baraza la Makanisa la Dunia na makanisa ya Mashariki na Magharibi, zichukue msimamo wa kibinadamu na wa kimaadili dhidi ya vita vya mauaji ya kizazi huko Ghaza.”

Wito huu umetolewa kwa madhumuni ya kusimamisha mara moja mashambulizi dhidi ya Ghaza, kuzuia uhalifu dhidi ya raia wasio na hatia na kusimama dhidi ya dhulma, na taasisi zinapaswa hasa Marekani na serikali za Magharibi wanaounga mkono wavamizi, zishinikizwe kusimamisha vita.

“Sisi kama wanazuoni wa Kiislamu, tunaziomba serikali ambazo zimelengwa katika mradi wa uvamizi wa Kizayuni zichukue wajibu wa kukabiliana na mipango ya adui na zichukue hatua za kivitendo na halisi za kuzuia na kukabiliana nazo, Kwa hivyo, mkutano huu katika kumbukumbu ya Umma utabakia kama wito wa kihistoria wa kuunganisha safu inayoangalia kadhia ya Ghaza, utekelezaji wa majukumu ya Kiislamu na kibinadamu ya kusaidia, kuunga mkono na kuwasaidia watu wa Palestina, katika njia ya kukomesha uvamizi na kufikia uhuru wa ardhi, utasajiliwa kama mwendelezo wa jitihada za Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni wa Kiislamu na Taasisi ya Wanazuoni wa Kiislamu, na pia mwanzo mpya.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha