Ijumaa 29 Agosti 2025 - 17:49
Mtazamo wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ndio mfumo bora zaidi wa kusongesha mbele umoja katika ulimwengu wa Kiislamu

Hawzah/ Zaidi alisema: Ayatullahul-Udhma Khamenei, mara kwa mara wamesisitiza kwamba kutukana vitakatifu vya madhehebu ya Kiislamu ni haramu, na mtazamo huu ndio mfumo bora zaidi wa kusongesha mbele umoja katika ulimwengu wa Kiislamu

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Hawza, kutoka Isfahan, Dkt. Zaidi, Rais wa Chuo Kikuu cha Lahore – Pakistan, mchana wa leo katika kikao chake na Rais pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Nahjul-Balagha Isfahan, huku akitoa shukrani kwa shughuli za kielimu na za utafiti za taasisi hiyo, alisema: “Nina shauku ya kushughulikia mada ya akili bandia na utawala wa Kialawi katika Kongamano la Nne la Kimataifa la Nahjul-Balagha, kwa sababu naamini kuunganisha mijadala ya kisasa ya ulimwengu na mafundisho ya Nahjul-Balagha kunaweza kutoa suluhisho jipya kwa uendeshaji wa jamii za Kiislamu.”

Akiashiria kwamba mshikamano kati ya nchi za Kiislamu leo ni haja isiyokanushika, alisema: “Nahjul-Balagha katika uwanja huu ina nafasi yenye athari kubwa na yenye kujenga, na inaweza kuwa chombo cha kuleta ukaribu kwenye nyoyo za Waislamu na kuondoa dhana potofu za kihistoria kati ya madhehebu ya Kiislamu, tunapaswa kujitahidi mafundisho ya kitabu hiki kitukufu yasambazwe zaidi katika jamii za Kiislamu ili hakika ya Uislamu iwasilishwe kwa usahihi duniani.”

Rais wa Chuo Kikuu cha Lahore – Pakistan, akionyesha wasiwasi wake juu ya mienendo ya baadhi ya mitazamo ya kigaidi nchini mwake, aliongeza: “Baadhi ya watu hujitokeza Pakistan kwa jina la walinganiaji wa dini, lakini badala ya kujenga mshikamano wanajishughulisha na kueneza mifarakano miongoni mwa Waislamu, watu hawa hujitambulisha kama walinganiaji wa Kishia, lakini kwa kutukana matukufu ya Ahlus-Sunna hawasababishi tu tofauti, bali pia hawana uwezo wa kuwavuta hata wasikilizaji.”

Akasema: “Tajiriba imeonyesha kwamba; mshikamano kati ya Waislamu na mijadala kama vile Nahjul-Balagha, kwa madhehebu yote ya Kiislamu na hata wasiokuwa Waislamu, ni ya kuvutia, mafundisho haya yanazidi mipaka ya kimadhehebu na ni mabashiri ya ubinadamu na mshikamano.”

Zaidi, akiashiria nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu, alisema: “Mbinu ya tabligh na kuunda mshikamano kati ya Waislamu inapaswa kuwa kwa mujibu wa maelekezo ya Ayatullahul-Udhma Khamenei, Yeye mara nyingi amesisitiza kwamba kutukana matukufu ya madhehebu ya Kiislamu ni haramu, na mtazamo huu ndio mfumo bora zaidi wa kusongesha mbele umoja katika ulimwengu wa Kiislamu.”

Akasistiza: “Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, husisitiza juu ya haja ya kuzingatia mambo ya pamoja kati ya madhehebu ya Kiislamu, hii ni ramani ya wazi ya njia kwa Umma wote wa Kiislamu ambayo iwapo itatekelezwa, njama nyingi za maadui za kuibua mifarakano zitafutika.”

Rais wa Chuo Kikuu cha Lahore – Pakistan alisema: “Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, kwa mtazamo wake wa kina na wa kimaono ya mbali, siku zote amesisitiza juu ya kuepukana na mifarakano, leo Waislamu wanahitajia zaidi ya wakati mwingine wowote kuufanya ujumbe huu kuwa dira ya shughuli zao za kidini, kisiasa na kijamii.”

Akatamka wazi: “Iwapo sisi Waislamu badala ya kuzingatia tofauti za kihistoria, tukaongozwa kwa msingi wa Nahjul-Balagha na maelekezo ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, tutaweza kushuhudia kuundwa kwa umma mmoja wa Kiislamu, njia hii haitakuwa na manufaa tu kwa Waislamu, bali pia kwa binadamu wote.”

Mwisho wa ujumbe

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha