Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah A‘rafi – Mkurugenzi wa hawza nchini Iran – katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Madaktari iliyofanyika katika ukumbi wa Najmeh Khatun (s.a) ndani ya Haram ya Hadhrat Fatimah Ma‘suma (s.a), kwa uratibu wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba na Shirika la Mfumo wa Madaktari, aliwashukuru waandaaji wa hafla hiyo na akasema: “Katika mahali hapa patakatifu, mbele ya Hadhrat Fatimah Ma‘suma (s.a), ni wajibu kwanza kuzungumza kuhusu Mtume mkubwa wa Uislamu, Yale ninayoyasema yameegemezwa kwenye riwaya na vyanzo sahihi vya Kiislamu vinavyomwelezea Mtume wetu mtukufu.”
Mtume na upeo wa maadili:
Mjumbe wa Baraza Kuu la Vyuo vya Kidini alisema: “Mtume (s.a.w.) pamoja na elimu na maarifa makubwa, na pamoja na uimara na uthabiti katika njia ya Mwenyezi Mungu, kipengele cha tatu cha shakhsia yake kilidhihirika katika maadili, sifa njema za Mtume ndio mionekano muhimu zaidi ya uwepo wake; kiasi kwamba zaidi ya sifa 100 za kitabia na kimaadili zimeelezwa katika riwaya.”
Ayatollah A‘rafi akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akikaa pamoja na watu, akishauriana nao, akipunguza swala kwa ajili ya kushughulikia mambo ya watu, hakuwa akitoa jibu la kukataa ila pale alipohisi kuasiwa Mwenyezi Mungu. Alikuwa na uso wa furaha na bashasha, hakuwa na huzuni kwa kupoteza mambo ya dunia, ila alikuwa akikasirika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee, hakuwa akilipiza kisasi, alikuwa mtu wa zuhudi, kukinai na maisha rahisi, alikaa ardhini, akalala ardhini, alifanya kazi zake mwenyewe, na alikaa na maskini na wanyonge.”
Sira na mwenendo wa Mtume:
Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi wa Dini (Majlisi Khobregan) alisema: “Pamoja na unyenyekevu na tabasamu, Mtume (s.a.w) alikuwa mwerevu sana, akiwajulia hali watu, alikuwa akihimiza wema na kujibu ubaya kwa nasaha, alikuwa na ukarimu usio na kifani, daima katika kumtaja Mwenyezi Mungu, na aliwapa watu wote katika kikao chake umuhimu sawa, mikutano yake ilikuwa ya heshima, haya na utukufu, alijiona kama baba mwenye huruma kwa wote.”
Imamu wa Ijumaa wa Qom aliongeza: “Mtume (s.a.w) alikaa na masikini na hakukataa mwaliko wao, alipokea zawadi, aliitukuza familia, na alimpa mwanamke heshima kubwa, alikuwa na udhu daima na aliheshimu usafi, alipenda manukato na aliwahimiza watu wawe wasafi, alikuwa msamehevu wa makosa ya watu, alifumbia macho aibu zao na hakuwahi kukatiza mazungumzo ya mtu yeyote.”
Mtume kama kilele cha ubinadamu:
Mkurugenzi wa hawza alisema: “Sifa zote hizi na tabia hizi zimethibitishwa katika vyanzo sahihi vya Kiislamu – vya Kishia na Kisunni, tunajivunia kwamba tunaishi katika madhehebu ya Mtume kama huyu, ambaye ni kioo cha elimu, jihadi na maadili; na lazima awe mfano wa daima katika jamii ya Kiislamu.”
Akaongeza kwa kusema: “Kushikamana na Mtume (s.a.w) ndiko kutakuokoa duniani na Akhera, Mtume alikuwa mfano wa maadili, uaminifu wa ahadi, na bashasha mbele ya watu.”
Ibn Sina (Avicenna) na urithi wa kielimu:
Ayatollah A‘rafi pia alimtaja Bu Ali Sina (Ibn Sina) kama kilele adimu katika historia ya binadamu na kiunganishi cha tamaduni mbalimbali kupitia fikra ya Kiislamu, alisema: “Tupo katika mji ambao alama yake ni Hadhrat Fatimah Ma‘suma (s.a), Mtume (s.a.w) pia, kama huyu bibi mtukufu, alikuwa akipokea udhuru, hakuwa akiwadhalilisha watu, na daima alikuwa thabiti katika ahadi na mikataba yake.
Alikuwa na uso mzuri na wenye mvuto, na alipowasili kwenye kikao, ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa salamu, na alipokuwa akiondoka, ndiye aliyekuwa wa mwisho kuaga, katika kuwapokea wageni alikuwa mstari wa mbele, na mbele ya watu wote alikuwa mchangamfu.”
“Bu Ali Sina alisema kwamba kabla ya kufikia umri wa miaka 20 alikuwa amejifunza sayansi zote za zama zake, Alikuwa kinara katika elimu zote, fikra zake zikawa kiunganishi cha tamaduni za kibinadamu, fikra ya Kiislamu na ulimwengu mpya, tunapaswa kujivunia mirathi na fahari zetu, lakini tusisimame pale; bali kwa kuhamasishwa na wao, twende kwenye upeo wa juu zaidi.”
Umuhimu wa jamii ya madaktari:
Akisisitiza nafasi ya jamii ya madaktari katika uimarishaji wa taifa, A‘rafi alisema: “Miongoni mwa nguzo kuu za nguvu ya kitaifa ni elimu na teknolojia, jamii ya madaktari, hasa wakati wa majanga ya kiafya na matukio ya hivi karibuni, imeonyesha kwamba afya ya wananchi ni moja ya misingi mikuu ya nguvu ya taifa.”
Aliendelea: “Katika dhoruba kama janga la corona, majanga ya kiasili na hata mashambulizi ya hivi karibuni, madaktari wetu walionesha uwezo wao wa kielimu, kiteknolojia na kitaaluma, hii ni sehemu muhimu ya nguvu za taifa na lazima ishukuriwe zaidi.”
Familia nguzo ya mafanikio katika jamii:
Imamu wa Ijumaa wa Qom alikumbusha pia nafasi ya familia kwa kusema: “Nawashukuru wake na watoto wa madaktari na wote wanaoiunga mkono jamii ya afya, kwani familia ina nafasi ya kuamua katika mafanikio ya kijamii, wanawake wetu wamesimama mstari wa mbele katika ukuaji na ustawi wa taifa.”
Changamoto za sasa na mshikamano wa kijamii:
A‘rafi pia aligusia mashambulizi ya hivi karibuni huko Gaza na kusema: “Wakati maadui wanajaribu kwa kila njia kuvunja heshima na nguvu ya Iran, ni lazima tuimarishe nguvu ya kielimu na kiteknolojia sambamba na mshikamano wa kijamii, jamii ya madaktari pia lazima kila mara izingatiwe kama jamii kubwa, yenye heshima na hadhi ya juu.”
Mwisho wa ujumbe
Maoni yako