Jumapili 17 Agosti 2025 - 14:47
Ataba Tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yatangaza idadi ya mazuwari waliohudhuria katika Ziara ya Arubaini mwaka huu

Hawza/ Ataba Tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imetangaza uwepo wa zaidi ya mazuwari milioni 21 kwenye maadhimisho ya ziara ya Arubaini, taarifa hii imetolewa kwa kutumia mfumo sahihi wa kuhesabu kielektroniki unaotegemea akili mnemba, kwa ajili ya kurekodi idadi ya waumini waliowasili Karbala Tukufu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Katibu Mkuu wa Ataba Tukufu ya Abbasi (a.s) siku ya Ijumaa, tarehe 20 Safar al-Khayr 1447 Hijria Qamari (sawa na 21 Safar nchini Iran), ikilingana na tarehe 15 Agosti 2025 Miladia (24 Mordad 1404 Hijria Shamsia), katika tamko rasmi ametangaza ushiriki wa mazuwari 21,103,524 katika ibada ya ziara ya Arubaini ya Imamu Husein (a.s).

Ataba Tukufu ya Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuhesabu idadi ya waumini waliowasili Karbala Tukufu, imetumia mfumo wa kisasa wa kuhesabu kielektroniki unaotegemea akili mnemba, mfumo huu uliwekwa katika njia kuu za matembezi ya mazuwari katika milango ya Haram Tukufu.

Sehemu ya tamko hilo inasema:

“Tunawasilisha mkono wa rambirambi kwa Hadhrat Hujjat ibn al-Hassan (a.t.f.s), kwa Marjaa wakuu wa dini, na kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu, hususan Iraq ardhi ya Manabii, Mawasii na Awliyaa – kutokana na mnasaba wa siku hizi za Arubaini ya Husein (a.s). Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aihifadhi ardhi ya Kiislamu na kuwarudisha waumini wa Aba Abdillah Husein (a.s) salama katika miji na nchi zao.”

Kama ilivyokuwa kwa zaidi ya karne kumi na tatu, Karbala Tukufu imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mazuwari wa Bwana wa Mashahidi, Imamu Husein (a.s), na ndugu yake mtukufu Abulfadhil Abbasi (a.s) katika msimu wa ziara ya Arubaini ya mwaka 1447 Hijria Qamari, huduma mbali mbali zimeendelea kutolewa kwa waumini na mazuwari, jambo ambalo ni miongoni mwa fahari za Atabat Tukufu, huduma hizo zinajumuisha za kitabibu, kijamii na maombolezo, pia mfumo wa kurekodi idadi ya mazuwari waliowasili Karbala kwa kutumia mfumo wa kielektroniki umeendeshwa kwa mwaka wa kumi mfululizo na Kitengo cha Mawasiliano na Usalama wa Taarifa cha Atabat Tukufu ya Abbasi (a.s), aidha, Kituo cha Taarifa na Utafiti wa Takwimu cha Kafeel kilibeba jukumu la kusimamia usajili wa takwimu za huduma zingine zote mjini Karbala.

Kwa mujibu wa mfumo wa kuhesabu kielektroniki unaotegemea akili mnemba, uliowekwa katika milango mikuu mitano ya kuingilia Karbala (barabara ya Baghdad–Karbala, Baghdad–Jamaliyya, Najaf–Karbala, Babil–Karbala, na Husayniyya–Karbala), idadi ya waumini waliowasili Karbala Tukufu kuanzia siku ya kwanza ya Safar al-Khayr hadi saa kumi na mbili jioni siku ya ishirini Safar al-Khayr mwaka huu, ilifikia 21,103,524 (milioni ishirini na moja, laki moja na tatu, elfu tano na mia mbili na ishirini na nne).

Katika tamko hilo pia, umetolewa mchoro wa kulinganisha takwimu na miaka iliyopita.

Ataba Tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yatangaza idadi ya mazuwari waliohudhuria katika Ziara ya Arubaini mwaka huu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha