Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi, katika khutba ya Ijumaa ya tarehe 24 Mordad (katika kalenda ya Kiirani), ilizofanyika katika Musalla Quds wa Qom Iran, akielezea harakati ya Arubaini ni nembo ya uchaji Mungu wa kiutendaji, alisema: Mapenzi kwa Imamu Hussein (a.s.) na malengo yake yamedhihirika katika ushiriki wa mamilioni ya waombolezaji wa Kishia kwenye maandamano ya Arubaini, hafla hii ni mahali pa kudhihirisha mapenzi ya Mwenyezi Mungu na uhusiano usiovunjika wa umma wa Kiislamu na malengo ya harakati ya Ashura, ambapo chanzo chake ni uchaji Mungu wa kweli.
Akinukuu aya ya 32 ya Suratu Al-Hajj:
«ذَٰلِكَۖ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ ٱللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى ٱلْقُلُوبِ»alisema: Yeyote atakayetukuza alama na nembo za Mwenyezi Mungu na kuziheshimu kwa vitendo, hiyo ni dalili ya uchaji Mungu wa dhati, Nembo za Huseiniyya, hususan matembezi ya Arubaini, ni miongoni mwa nembo bora kabisa za Mwenyezi Mungu.
Imamu wa Ijumaa wa Qom alisema: Arubaini ni jina la siri na alama ya kudumu kwa mapambano ya Huseiniyya, yaliyopangwa kwa ajili ya kuandaa ulimwengu kwa kudhihiri kwa Mlipiza kisasi wa Ahlul Bayt (s.a.w.). Harakati ya Imamu Hussein (a.s.) katika Ashura iliondoa hatari kubwa iliyokuwa ikiutishia Uislamu, mapambano ya Huseiniyya yaliweza kuzuia kushuka, kuasi na kurejea kwenye zama za ujahiliyyah.
Khatibu wa Ijumaa wa Qom alieleza: Matembezi ya Arubaini ni maandamano makubwa zaidi duniani dhidi ya mfumo wa ukafiri na ubeberu, iwapo yatafafanuliwa, kufahamishwa na kutekelezwa ipasavyo, basi ni istighatha ya kimataifa kwa Mwenyezi Mungu ili kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f.).
Mwakilishi wa Waliyyul Faqih Qom aliongeza kuwa: Arubaini ni harakati ya pamoja kuelekea kwa Imamu na Hujjah wa Mwenyezi Mungu, Arubaini ina uhusiano wa karibu mno na Mahdawiyya, kiasi kwamba Labbaik ya Hussein ni sawa na Labbaik ya Mahdi.
Akasema: Moja ya masomo muhimu ya Arubaini ni kuwatambua maadui wa haki na Uislamu katika zama hizi, ni lazima katika zama hizi tuwatambue kina Yazidi wa wakati huu, hata leo wapo watu wanaotambulika kwa sifa za wauaji wa Imamu Hussein (a.s.) na wanaendeleza shughuli zao, mfumo wa ubeberu wa kimataifa, Marekani muuaji, utawala wa kizayuni wa kughushi, wanafiki wa eneo hili na wanaosuluhisha na utawala wa kizayuni muonevu—kwa mtazamo wa Uislamu—wanahesabiwa kuwa miongoni mwa watekaji na wauaji wa Imamu Hussein (a.s.).
Khatibu wa Ijumaa wa Qom alikumbusha kuwa: Ushiriki wa makundi mbalimbali ya watu kutoka nchi mbalimbali katika kongamano kubwa la Arubaini ni fursa bora ya kubainisha na kutangaza Uislamu safi wa Muhammadi.
Akasema: Ibn Qaulawayh katika kitabu K'amiluz-Ziyarah amepokea kwamba mtu atakayetembea kwa miguu kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s.), Mwenyezi Mungu humwandikia mema kwa kila hatua, humfutia dhambi moja na humuinua daraja moja.
Mlezi wa Haram ya Hadhrat Fatimah Ma‘suma (s.a.) akigusia Siku ya Kimataifa ya Msikiti alisema: 30 Mordad ni kumbukumbu ya uvunjaji heshima uliofanywa na Wazayuni mwaka 1348 SH, ambapo waliteketeza moto Qibla ya kwanza ya Waislamu, yaani Msikiti wa Al-Aqswa.
Akasema: Kaumu hii ya Kiyahudi, kwa sababu ya itikadi yao batili, vitendo vyao batili, matendo kinyume na haki na chuki dhidi ya haki na uadilifu, mara nyingi katika Qur’ani imekashifiwa na kulaaniwa, kundi hili halimuheshimu Mwenyezi Mungu, Mtume, Kitabu cha Mwenyezi Mungu, misikiti na watu.
Ayatullah Saidi katika khutba ya kwanza, akigusia aya ya 18 ya Suratu Fussilat:
«وَنَجَّيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ»(Yaani: Wale waliomuamini na wakawa wanamcha Mwenyezi Mungu tuliwaokoa), alisema: Kutekeleza wajibu, kushikamana na halali na haramu za Mwenyezi Mungu, na kuokoka na ghadhabu na adhabu Yake kunategemea uchaji Mungu.
Akaendelea kwa kusema: Wale wanaoamini na kudumu katika uchaji Mungu wako salama na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, Muumini asiye na uchaji Mungu au mwenye uchaji Mungu dhaifu ni kama gari lisilo na breki—lina motisha na chombo cha kutembea, lakini likikumbana na hatari halina uwezo wa kusimama.
Akasema: Mwenyezi Mungu katika aya ya 124 ya Suratu Tawba anagusia mwitikio wa waumini mbele ya kushushwa kwa aya za Mwenyezi Mungu:
«وَإِذَا مَا أُنْزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُمْ مَنْ يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَذِهِ إِيمَانًا فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ»(Yaani: Pindi inapoteremshwa sura, wapo miongoni mwao wanaosema: Ni nani kati yenu ambaye sura hii imemuongezea imani? Lakini wale waliomuamini imewaongezea imani na wanasherehekea).
Mlezi wa Haram ya Hadhrat Fatimah Ma‘suma (s.a.) alisisitiza kwa kusema: Kwa mujibu wa aya hii, kushushwa kwa aya za Mwenyezi Mungu kwa waumini kuna faida mbili: kuongeza imani na kufurahisha.
Akaeleza: Katika aya ya 125 ya Suratu Tawba, Mwenyezi Mungu anaeleza mwitikio wa wanafiki mbele ya kushushwa kwa aya:
«وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَى رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا وَهُمْ كَافِرُونَ»(Yaani: Ama wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi, imewaongezea uchafu juu ya uchafu wao na wamekufa wakiwa makafiri).
Imamu wa Ijumaa wa Qom akaendelea: Kwa mujibu wa aya hii, kushushwa kwa aya za Mwenyezi Mungu kwa wanafiki kunasababisha kuongezeka kwa uchafu juu ya uchafu wao na kufa wakiwa makafiri, yaani kadiri aya zinavyoshuka, ndivyo uchafu wao unavyoongezeka.
Akasema: Mwenyezi Mungu ameeneza meza ya rehema ya Qur’ani kwa watu wote, Ikiwa mtu ana nafsi yenye afya hatopatwa na maradhi mabaya ya unafiki, na kwa matokeo hayo atapata neema ya Mwenyezi Mungu, lakini mvua—ambayo ni rehema ya Mwenyezi Mungu—ikidondoka kwenye shimo lenye mzoga, haiondoi harufu mbaya bali huiongeza.
Khatibu wa Ijumaa wa Qom alisema: Kuambukizwa na dhambi na maasi, na kuambukizwa na unafiki, vyote ni maradhi, lakini kuambukizwa na dhambi ni ugonjwa usio mbaya sana, ambao unaweza kutibika kwa toba na kuzingatia, lakini kuambukizwa na unafiki ni kama maradhi sugu mabaya ambayo yasipotibiwa mapema humuangamiza mtu na husababisha afe akiwa kafiri.
Mwisho wa ujumbe
Maoni yako