Ijumaa 15 Agosti 2025 - 10:13
Taarifa ya Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom Irani [J'amiatul Mudarris'in] Kuhusiana na Kulaani Mpango wa Kuzuia na Kuuteka Kikamilifu Ukanda wa Ghaza / Aibu iliyowapata  waongo wanaodai haki za Binadamu

Hawza/ Mpango dhalimu na kinyume cha ubinadamu wa kuiteka Ghaza kwa hakika utashindwa, na mapambano ya Kiislamu huko Ghaza, kwa idhini na msaada wa Mwenyezi Mungu, yatapats ushindi wa mwisho katika uwanja huu, InshaAllah.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, kufuatia mpango wa kuimarisha vizuizi na kuuteka kikamilifu Ukanda wa Ghaza na utawala ghasibu wa Kizayuni, Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom Irani, imetoa taarifa ifuatayo:

Bismillahir Rahmanir Rahim

Matukio ya kumwaga damu huko Ghaza na mauaji ya kimbari ya kusikitisha ya watu wanyonge wa eneo hilo kwa kuzingirwa na kuzuiwa bidhaa za chakula bado yanaendelea, wauaji katili wa watoto, chini ya kivuli cha msaada wa wazi na wa siri wa Marekani na uzembe wa taasisi za kimataifa na mashirika ya haki za binadamu, bila woga na kwa ujeuri, wanaendeleza mipango ya kuimarisha vizuizi na kuuteka kikamilifu Ukanda wa Ghaza, Sheria zote za kivita na mikataba ya haki za binadamu zinatambua vitendo vya utawala ghasibu wa Kizayuni kuwa ni mfano halisi wa ugaidi wa kiserikali, uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari.

Wapenda uhuru duniani kote pia wamejitokeza mitaani kuunga mkono watu wanyonge wa Palestina na watoto waliokumbwa na mzingiro wa risasi na njaa; lakini ukimya wa serikali vibaraka, shinikizo la mabaraza ya Kizayuni, na uovu wa viongozi wa dola za kibeberu, ni kizuizi cha kufikiwa kwa makubaliano yoyote ya kusitisha vita na kuwakomboa watu wa Ghaza.

Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom, ikifuata mafundisho ya Kiislamu na mikakati ya ki-Mungu na ya kimaantiki ya Maimamu wawili wa Mapinduzi, inasisitiza juu ya kuunga mkono kwa kudumu watu wa Palestina na malengo ya Quds Tukufu, na inatangaza:

Desturi za Mwenyezi Mungu na historia ya mataifa ambayo, kwa kutegemea msaada wa Mungu, imesimama imara katika njia ya haki, inaonyesha kuwa ushindi na msaada wa ki-Mungu utatimia hivi karibuni, na ushindi utakuwa upande wa haki na wa watu wanyonge, madhalimu wa kifirauni hatimaye wataangamia katika dimbwi la dhuluma na uhalifu wao, na aibu itabaki kwenye nyuso za wale wanaowaunga mkono wahalifu na wadai wa haki za binadamu ambao wamefeli katika uwanja huu.

Leo Ghaza ni uwanja wa majaribio kwa dhamira zilizo macho na zenye ufahamu; na ukimya wowote mbele ya dhulma kubwa na kinyume cha utu inayofanywa na Wazayuni ni ushirikiano na utawala huo katili na mchafu, mpango dhalimu na kinyume cha utu wa kuiteka Ghaza kwa hakika utashindwa, na mapambano ya Kiislamu huko Ghaza, kwa idhini na msaada wa Mwenyezi Mungu, yatapata ushindi wa mwisho katika uwanja huu, InshaAllah.

{...وَسَیَعلَمُ ٱلَّذِینَ ظَلَمُوا۟ أَیَّ مُنقَلَب یَنقَلِبُونَ }

"Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka."

[Surah Ash-Shuʿarāʾ: 227]

Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha