Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, sambamba na wingi mkubwa wa mazuwari wa Arubaini ya Husein (a.s.) wanaotoka Najafu Ashraf kuelekea Karbala al-Mualla, katika nguzo ya 794 kumewekwa hema ambalo limejipa jukumu la uelimishaji wa kisiasa na kufichua sura halisi ya nguvu za mabeberu.
Hema hili, kwa muundo unaofanana na banda la maonyesho, kuta zake zimefunikwa na mabango makubwa yanayoonesha jinai zinazofanywa utawala wa Kizayuni na Marekani. Picha, vielelezo na nyaraka zilizowekwa wazi vinajumuisha mandhari ya mauaji ya watoto na raia wasio na hatia wa Kipalestina, uharibifu uliofanywa Yemen na maafa mengine ya kibinadamu yanayoashiria nafasi ya moja kwa moja ya wahalifu hawa ndani yake.
Mbali na maonyesho ya kuona, wanafunzi wa hawza na wahubiri waliopo katika hema hili, kwa kutoa uchambuzi na simulizi za kihistoria, wanabainisha yaliyo nyuma ya pazia ya matukio haya kwa mahujaji, Simulizi hizi hufanyika kwa lugha mbalimbali, na maeneo ya hema kutokana na uwepo wa wageni kutoka mataifa tofauti hupata sura ya kimataifa.
Kwa mujibu wa waandaaji, lengo kuu la hatua hii ni kuamsha fikra za umma na kuunganisha maana ya kiroho ya Arubaini na uwajibikaji wa kijamii na kisiasa katika ulimwengu wa Kiislamu, wengi wa mazuwari pia, kwa kusimama muda mrefu mahali hapa, sambamba na kupongeza ubunifu wa waandaaji, wametoa msisitizo juu ya ulazima wa kueneza shughuli kama hizi katika njia nyingine za Arubaini.
Hema hili ni mfano wa namna ambavyo mkusanyiko mkubwa zaidi wa kila mwaka wa Waislamu unaweza kugeuzwa kuwa chombo cha kufichua dhulma na kubainisha ukweli.
Maoni yako