Jumapili 3 Agosti 2025 - 00:53
Uholanzi yampiga marufuku Ben Gvir kuingia nchini humo

Hawza/ Vyombo vya habari vya Uholanzi vimetangaza kuwa serikali ya nchi hiyo imeamua, katika muktadha wa kuongeza shinikizo kwa utawala wa Israel ili iachane na vikwazo vya chakula na maji huko Ghaza, kumuwekea vikwazo Waziri wa Mambo ya Ndani wa mrengo mkali wa kulia, Ben Gvir, na Smotrich.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, vyombo vya habari vya Uholanzi vimetangaza kuwa serikali ya nchi hiyo imeamua, kwa lengo la kuongeza shinikizo kwa utawala wa Israel ili iachane na vikwazo vya chakula na maji huko Ghaza, kumuwekea vikwazo Waziri wa Mambo ya Ndani wa mrengo mkali wa kulia, Ben Gvir, na Smotrich.

Serikali ya Uholanzi pia imemuita Modi Ephraim, mwakilishi wa Israel nchini humo, na kulaani kuzingirwa kwa Ghaza kunakofanywa na utawala huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi, katika maandishi yaliyomo kwenye magazeti ya Kiholanzi ya "Algemeen" na "Dagblad", yamesema kuwa hatua hii dhidi ya Ben Gvir na Smotrich imechukuliwa kwa sababu watu hawa mara kwa mara kupitia majukwaa yao wamekuwa wakitaka kufanyika kwa mauaji ya kimbari huko Ghaza! Wamewekewa vikwazo na serikali ya Uholanzi na hawana haki ya kuingia nchini humo.

Tamko hili ni ushahidi wa hivi karibuni zaidi wa kuongezeka kwa mvutano kati ya Israel na Umoja wa Ulaya, hali ambayo imetokana na ripoti za kutia wasiwasi kuhusu hali ya dharura iliyoko Ghaza, Waziri Mkuu wa Uholanzi, Dick Schoof, na Rais wa nchi hiyo, Isaac Herzog, wameeleza waziwazi upinzani wao dhidi ya uzembe wa kisiasa wa Israel.

Chanzo: Shirika la Habari The Times of Israel

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha