Jumanne 29 Julai 2025 - 21:31
Hawza za kielimu Pakistan, zatangaza kushikama na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Hawza/ Mkurugenzi wa Jami’atul-Urwatul-Wuthqa mjini Lahore, Pakistan, katika ujumbe aliomtumia Ayatollah A’rafi, Mkurugenzi wa Hawza, ametoa pongezi kwa kushindwa kwa maadui katika vita vya kulazimishwa vya siku kumi na mbili, na kutangaza kuwa, hawza za Pakistani zinaunga mkono kikamilifu malengo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya habari za kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Jawad Naqawi, Mkurugenzi wa Jami’atul-Urwatul-Wuthqa mjini Lahore, Pakistan, kupitia ujumbe aliomtumia Ayatollah A’rafi, Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, sambamba na kusisitiza uungaji mkono wa maulamaa na wananchi ya Pakistan malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu, ameonesha shukrani na kutoa pongezi zake kwa ushindi wa kimungu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kukabiliana na ubeberu wa kimataifa na kushindwa kwa maadui, hususan katika vita vya kulazimishwa vya siku kumi na mbili.

Matini kamili ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

بسم الله الرحمن الرحیم

Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah A’rafi

السلام علیکم و رحمة الله و برکاته

Katika historia, daima kumekuwa na makundi mawili yanayokabiliana: "waliodhulumiwa na wadhulumu". Madhalimu wamekuwa wakivamia wadhulumiwa, wakijaribu kuwatia nguvu na kuwatumikisha, lakini waliodhulumiwa, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu, wameonesha msimamo na ujasiri katika kukabiliana nao na wamesimama imara.

«وَلَمَّا بَرَزُواْ لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ قَالُواْ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَینَا صَبۡرࣰا وَثَبِت أَقدَامَنَا وَٱنصُرنَا عَلَی ٱلقومِ ٱلکَٰفِرِینَ»

Na walipo toka kupambana na Jaluti na majeshi yake walisema: Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri
(Baqara: 250)

Katika zama za sasa, baada ya ushindi wa kishujaa wa Mapinduzi ya Kiislamu chini ya uongozi thabiti na wa kishujaa wa mtu mkubwa wa historia, Imam Khomeini (r.a), mapambano haya yamechukua nguvu zaidi, na maadui walioapa na wanyonyaji wa dunia wamekusudia kuyashambulia Mapinduzi ya Kiislamu kwa hila zao za kinyama.

Mapinduzi ya Kiislamu, kwa kutoa na kuthibitisha fikra ya Uislamu halisi ambayo imekuwa chanzo cha mwamko na uhuru kwa wanadamu huru, yamekabiliana na ubeberu wa kimataifa na kuupigsha magoti, nuru ya Mapinduzi ya Kiislamu inaendelea kuenea siku baada ya siku, ikiwa chanzo cha matumaini na mwamko wa mataifa yote yaliyodhulumiwa, hususan taifa la Palestina lililodhulumiwa.

Ubeberu wa kimataifa, ukiongozwa na Marekani mnyonyaji wa dunia, kutokana na kuogopa fikra ya kimataifa ya Mapinduzi ya Kiislamu, daima umekuwa ukijitahidi kuzuia kuenea kwake na kwa kufanikisha lengo hili ovu, haujawai kuacha kufanya jinai na khiyana, daima wamekuwa wakipanga njama dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu, hususan Iran, na kuendelea na ukatili na uporaji wao.

Miongoni mwa jinai za hivi karibuni ni vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na Israel na Marekani mnyonyaji wa dunia dhidi ya Iran, ambapo walishambulia "Ummu al-Qura" wa ulimwengu wa Kiislamu na moyo wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Shetani mkubwa, Marekani mnyonyaji wa dunia, kwa kushirikiana na utawala wa Kizayuni mporaji, baada ya kufanya jinai mfululizo huko Palestina, Lebanon, Syria na Yemen, ulianzisha vita vya kulazimishwa dhidi ya Iran, na kwa dhana zao batili walitarajia ushindi katika vita hivyo.

Lakini, kwa matakwa ya kimungu, maelekezo yenye hekima na ujasiri na msimamo thabiti wa Kiongozi wa Waislamu, Mtukufu Ayatollah al-Udhma Imam Khamenei (Mola amuhifadhi), mshikamano na umoja wa wafuasi wa wilaya, pamoja na juhudi na msimamo wa wapiganaji wa Kiislamu, mpango wao mchafu ulivunjwa na walishindw, hali hii iliionesha dunia nguvu ya uongo ya Shetani mkubwa na washirika wake, na ukweli wa kufeli kwa Israel mporaji, na ikawaletea udhalili na aibu katika uwanja wa kimataifa.

«کَمْ مِنْ فِئَةٍ قَلِیلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً کَثِیرَةً بِإِذْنِ اللَّهِ وَاللَّهُ مَعَ الصَّابِرِینَ»

Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.

(Baqara: 249)

Nguvu na uweza wa Iran umeitia dunia katika mshangao na kuwa chanzo cha heshima na utukufu wa mfumo wa Kiislamu, na umeimarisha uthabiti, mshikamano na umoja katika ulimwengu wa Kiislamu.

«مَنْ کانَ یرِیدُ اَلْعِزَّةَ فَلِلّهِ اَلْعِزَّةُ جَمِیعاً»

Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu.

(Faatir: 10)

Tunatoa pongezi kwa ushindi huu ulio wazi na nusra ya kimungu, na tunatoa rambirambi kutokana na kupata shahada makamanda wa kishujaa wa Kiislamu, wanasayansi mashujaa, na wanawake na watoto wasio na hatia waliokunywa kikombe cha shahada katika vita hivi vya siku kumi na mbili, kwa heshima ya Imam al-Asr (aj), Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Mheshimiwa Ayatollah al-Udhma Imam Khamenei (Mola amuhifadhi),  na taifa lote la mashahidi la Iran.

Hawza za Kielimu za Pakistan, maulamaa na tabaka mbalimbali za wananchi, katika kulinda na kuhifadhi malengo ya Imam (r.a) na Kiongozi Mtukufu (Mola amuhifadhi), na mafanikio ya thamani ya Mapinduzi ya Kiislamu, daima wamekuwa mstari wa mbele, na katika nyakati ngumu na matatizo yaliyowakumba Iran na umma wa Kiislamu, wamekuwa wakionesha uungaji mkono wa kila namna na msaada wa kisiasa, kidini na kimaadili, daima wamesimama pamoja na taifa la Iran hadi mwisho, na katika siku zijazo pia watabakia waaminifu kwa thamani za kidini na za kimapinduzi, wakisikiliza maelekezo ya Kiongozi wa Waislamu Mtukufu Imam Khamenei (Mola amuhifadhi), na hawataacha lolote, wakiwa tayari zaidi kwa kujitoa muhanga na kujitolea.

Aidha, katika wakati huu, tunakuhakikishia kuwa, kama tulivyoweka mbele kufafanua fikra za Imam mwanzilishi na Kiongozi Mtukufu wa Mapinduzi, kueneza malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu, kueneza utamaduni wa kidini na kimapinduzi, na kulinda na kutetea thamani na mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu, vivyo hivyo katika siku zijazo, kwa uthabiti na uimara zaidi, tutaendeleza njia hii tukufu, na tutaendelea kusimama imara na kwa azma thabiti zaidi mbele ya maadui wake, kwani huu ni wajibu wetu wa kidini na kimapinduzi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mkarimu nusra ya mwisho ya haki dhidi ya batili, maisha marefu ya Kiongozi wa Waislamu Mtukufu Imam Khamenei (Mola amuhifadhi), na mafanikio ya kila siku ya wapenda mfumo mtukufu wa Kiislamu, hususan wewe Mheshimiwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Jami’atul-Urwatul-Wuthqa
Lahore – Pakistan
Sayyid Jawad Naqawi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha