Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, ofisi ya Marjaa mkubwa, Mtukufu Ayatollah Al-Udhma Sayyid Ali Husaini Sistani huko Najaf Ashraf, imetoa taarifa kuwa, leo Jumamosi, tarehe 26 Julai 2025 (4 Mordad 1404) itakuwa siku ya mwisho ya mwezi wa Muharram al-Haram, na Jumapili [kwa mujibu wa mabna yake katika kuthibitisha kuona hilali kwa jicho la kawaida] itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Safar mwaka 1447 Hijria Qamaria.
Ni vyema kutaja kwamba, ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi, Ayatollah Al-Udhma Khamenei, imetangaza kuwa katika jioni ya Ijumaa, mwezi umeonekana kwa kutumia vifaa katika baadhi ya maeneo, na kwa mujibu wa mabna yake, siku ya Jumamosi itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Safar.
Maoni yako