Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hazrat Ayatollah Nouri Hamedani katika kikao na baadhi ya wanazuoni wa Hawza ya kielimu ya Qom, huku akinukuu siku za mwezi wa Muharram, aliutaja wakati wa miezi ya Muharram na Safar kuwa ni muda wa kipekee kwa ajili ya kufanya tablighi, na akasema: Lazima tuelewe kuwa Hawza haipaswi kubaki nyuma katika maendeleo ya kielimu na nyanja za mitandao ya kisasa, bali lazima ifanye kazi kwa njia ya kisasa. Hali ya leo si kama miaka michache iliyopita, kizazi cha leo kina mtazamo tofauti, kwa hiyo mhubiri lazima awe mwanazuoni mahiri na mwenye maadili ya hali ya juu.
Ayatullah Nouri Hamedan huku akisisitiza juu ya ulazima wa kujibu shubha na kuepuka kauli zisizo na ushahidi wala maudhui, alikumbusha kuwa: Leo watu wanatarajia tuwe watu wa kutoa majibu ya shubha na matatizo yao, si kwamba tuwazuge kwa kauli zisizo na msingi wala mashairi yasiyo na maudhui. Leo hatuna uhaba wa wahadhiri na waimbaji wa maombolezo wa kweli, lakini baadhi yao kwa jina la wahadhiri au waimbaji huzungumza mambo yasiyo na ushahidi wala chanzo. Lazima tuwatangaze Ahlul-Bayt (as) kwa maneno yao wenyewe.
Kiongozi huyu wa kidini akaendelea kusema: Leo watu wanatarajia kutoka kwetu mafunzo ya dini yaliyo sahihi na yenye ushahidi, na kwa ajili ya jambo hili ni lazima mtu ajitahidi. Tusifikiri kuwa kuvaa ‘aba (joho) na kuswali swala ya jamaa kisha kutoa hotuba moja basi ni kutimiza wajibu, halafu tusijihusishe na watu, watu wa leo wanataka sisi tuwe sauti yao na watetezi wa haki zao, kwa hiyo Sheikh aliyevaa joho lazima aelewe mahitaji ya jamii.
Hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuzungumza kwa mtazamo wa udhaifu ndani Jamhuri ya Kiislamu na kudhoofisha heshima ya watu, kisha licha ya usaliti na uhalifu wa maadui, bado yeye akaendelea kuwaamini tena.
Mtukufu huyo aliendelea kwa kueleza umuhimu wa kuwa “mwanazuoni anayejua zama zake” na akaongeza kwa kusema: Pale ambapo Mtukufu alisema:
«العالِمُ بِزَمانِهِ لا تَهجُمُ عَلَیهِ اللَّوابِس.»
Mwanazuoni anayejua zama zake hatadanganywa na mchanganyiko wa mambo
Maana yake nini? Sifa muhimu zaidi ya mwanazuoni anayejua zama zake ni kutambua matukio ya wakati wake. Leo mtu anasononeka sana anapoona kwamba ulimwengu wote wa ukafiri na unafiki umeungana ili kuiangamiza dini, lakini bado baadhi wanakaa kimya, mwanazuoni anayeshuhudia dini inavyoteketea na bado akabaki asiyejali, huyo si mwanazuoni.
Kiongozi huyu wa kidini kwa kuitukuza subira na ustahimilivu wa watu wa Iran katika vipindi vyote, hasa wakati wa vita vya kulazimishwa, alisisitiza kwa kusema: Hakika watu hawa waliwapiga maadui mdomoni, na kwa kweli waliuonyesha ulimwengu kuwa ni watu wa utamaduni wa kale, na mioyo yao imo katika Uislamu na Ahlul-Bayt ‘alayhim as-salam.
Maoni yako