Jumapili 13 Julai 2025 - 23:04
Lengo la juu kabisa la kuwa faqihi katika dini ni kuwaonya watu / Uhusiano wa kina kati ya muqawama wa taifa la Iran na harakati ya damu ya Ashura

Hawza/ Mkurugenzi wa vyuo vya kidini (hawza) Irani amebainisha kuwa: Katika hali ya hatari ya sasa ambapo maadui wameushambulia kwa nguvu zote na kila upande mfumo mtukufu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, uhusiano usiovunjika kati ya maana ya Ashura katika kupambana na batili na jihadi ya kubainisha haki umejitokeza zaidi kuliko wakati wowote ule.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa Ayatollah Alireza A'rafi, Mkurugenzi wa Vyuo vya Kidini vya Nchini Irani, ni kama ifuatavyo:

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

الَّذِینَ یُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّهِ وَیَخْشَوْنَهُ وَلَا یَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّهَ ۗ وَکَفَیٰ بِاللَّهِ حَسِیبًا

Utamaduni wa damu ya Ashura na harakati kubwa ya Imam Hussein daima umekuwa chemchemu inayochemka ya kuamsha mwamko, upeo wa ndani (basira) na muqawama katika historia nzima. Mwezi wa Muharram si tu sehemu muhimu ya kalenda ya Kishia, bali ni fursa isiyo na kifani kwa ajili ya kusoma upya na kubainisha maadili ya milele ya Kiislamu, kusimama dhidi ya dhulma, na kufichua ukweli.

Katika hali nyeti ya sasa ambapo maadui waumeshambulia kwa nguvu zote na kila upande mfumo mtukufu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, uhusiano usiovunjika wa maana ya Ashura katika kupambana na batili na jihadi ya kubainisha haki umejitokeza wazi zaidi, na siku za Muharram zimekuwa ni uwanja muwafaka wa kuangazia fikra za umma na kuimarisha moyo wa kusimama imara dhidi ya mashambulizi ya kiutamaduni na vyombo vya habari, kwa lengo la kuitikia wito wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (Mola amuhifadhi) kuhusu ulazima wa jihadi ya kubainisha ukweli, kuielimisha jamii na kufikisha ujumbe kwa njia bayana.

Katika mazingira haya, safari ya idadi kubwa ya vipaji bora kutoka katika hawza, ambao wameuelewa umuhimu wa tablighi na kwa usahihi wametambua kuwa lengo la juu kabisa la kuwa faqihi ni kuwaonya watu, na ambao kwa muundo wa makundi ya tablighi na kwa kutumia mbinu mpya za uenezi wamejitahidi kuzuia mashambulizi ya mseto ya adui, ni jambo la kusifiwa.

Mimi binafsi natangaza shukrani zangu kwa juhudi za watekelezaji wote wa tablighi wa hawza, na hasa kwa jamii ya wasomi na vipaji bora vya hawza, katika kutambua wakati mwafaka kwa ajili ya kuipa matumaini jamii na kubainisha uhusiano wa kina kati ya muqawama wa taifa la Iran na harakati ya damu ya Ashura, na pia ninawashukuru kwa jitihada zao wale wote walioshiriki katika harakati hii ya kusifiwa ndani ya kambi ya vita ya mseto ya “Balagh-e-Mubin” (ufikishaji wa wazi), Idara ya Tablighi na Masuala ya Kiutamaduni, na Ofisi ya Masuala ya Wasomi na Vipaji Bora.

Natumaini kuwa harakati hii yenye thamani itaendelea katika misimu ya tablighi ijayo, na “tablighi” – kama alivyoeleza Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika ujumbe wake wa thamani katika mkutano wa maadhimisho ya miaka mia moja ya Hawza ya Qom, na matamshi mengine muhimu ya mtukufu huyo – itapewa kipaumbele cha kwanza ndani ya hawza.

Alireza A'rafi
Mkurugenzi wa Vyuo vya Kidini Irani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha