Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza,, katika hafla hii Hujjatul-Islam Mas'ud 'Ālī alitoa hotuba ambayo ilielezea funzo la harakati ya Imam Hussein (as) kuhusiana na kusimama kidete pamoja na kustahimili dhulma. Alilitaja taifa la Kiislamu la Iran kuwa ni mhimili wa upande wa kimataifa wa muqawama chini ya uongozi wa Waliyyu Amr al-Muslimin (Kiongozi wa Waislamu), na akasisitiza kuwa Uzayonisti wa kimataifa ndio mhimili mkuu wa upande wa batili.
Alisema pia: “Taifa la Iran, kwa mujibu wa mafunzo ya Ashura, halitowahi kujisalimisha kwa upande wa batili; kwa sababu kauli mbiu ya "Uwe mbali kwetu ni udhalili" 'هیهات منا الذلة' ndilo somo lifuatwalo.”
Katika mwendelezo wa hafla hii, Bwana Mahmoud Karimi alisoma mashairi na maombolezo kwa ajili ya kumuomboleza Bwana wa Mashahidi, Abā 'Abdillāh (as), na mashujaa wenzake waliouawa kishahidi, akifanya marthiya (tenzi za maombolezo) kwa hisia na huzuni.
Maoni yako