Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza Arafi, Mkurugenzi wa hawza nchini Irani, katika mazungumzo yake na shirika la habari la Hawza, ameeleza kuwa kuwa tupo katika siku nyeti sana na za kipekee za nchi na katika moja ya sehemu za mabadiliko muhimu katika historia tukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu, na kwa kuitukuza kumbukumbu ya mashahidi na Imamu wa mashahidi, na kwa kuthamini na kushukuru vikosi vya ulinzi na taasisi zote ambazo zimejitolea katika kulinda nchi ya Kiislamu na kuandaa maandalizi ya kukabiliana na adui mwenye chuki, amesema: “Hasa ni lazima kuwashukuru watu wakuu, vijana waadilifu, wanawake na wanaume jasiri na mujahidina waliofanya mambo ya kushangaza kwa uwepo wao.”
Ameongeza kuwa: “Katika siku hizi, uwepo wa mara kwa mara wa watu wetu wakuu kote nchini Iran, kwa mshikamano na uangalifu wa hali ya juu na wa kina, pamoja na fahari ya kishujaa, umekuwa ni sababu ya kujivunia kwa Iran na Uislamu. Ni lazima kuwashukuru mmoja mmoja nyinyi wanaume na wanawake wa Iran, vijana jasiri na watetezi wa nchi.”
Maoni yako