Jumamosi 21 Juni 2025 - 18:41
Kuwauwa Viongozi wa Dini wajumbe wa baraza la umoja ni Uvunjaji wa wazi wa misingi ya Kimataifa

Hawza/ Viongozi wa juu wa dini Irani, katika muendelezo wa uvamizi wa Israil kuivamia Jamhuri ya kiislamu ya Irani wamesema kuwa; kutishia kuwauwa viongozi wa kisiasa na kidini katika nchi yeyote ile ambayo ni mwanachama wa umoja wa kimataifa, ni kuvunja kuliko wazi kwa misingi ya haki za kibinadamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Viongozi wa juu wa dini Irani, katika muendelezo wa uvamizi wa Israil kuivamia Jamhuri ya kiislamu ya Irani wamesema kuwa; kutishia kuwauwa viongozi wa kisiasa na kidini na vitisho vya Trump dhidi ya kiongozi wa mapinduzi, wametoa ujumbe wao kama ifuatavyo;

Kwa jina la Mungu Mmoja

Viongozi wa kidini na maulamaa wa dini ni taswira halisi ya utambulisho wa wafuasi wa dini za mbinguni, na kushambuliwa kwao ni sawa na kushambulia imani na hisia za mamilioni ya watu na ni tishio kwa uwepo wa kiroho na ustaarabu wa jamii.

Kwa misingi hii, na kwa kuzingatia mafundisho ya kidini na misingi ya wazi ya sheria za kimataifa, sisi — wawakilishi wa wanazuoni, wahadhiri na watafiti wa dini pamoja na wafuasi wa jamii za wachache wa kidini nchini Iran — tunatoa tamko hili kwa pamoja, tukieleza wasiwasi mkubwa juu ya matamshi ya chuki na vitisho visivyo na mfano vilivyotolewa na Rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei.

Tunapaza sauti yetu kwa viongozi wa dini duniani, taasisi za kimataifa, serikali na mataifa huru ya dunia kuhusu mambo yafuatayo:

1. Uvunjaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na Sheria za Kimataifa:

Vitisho vya kutaka kuwaua viongozi wa juu wa kisiasa na kidini wa nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa ni ukiukaji wa wazi wa Katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria za lazima za kimataifa, na ni kinyume na misingi ya haki za binadamu na sheria za kivita. Vitisho kama hivi vinastahili kuchukuliwa hatua za kisheria, na pale vinapokuwa karibu kutekelezwa, hutoa haki ya kujilinda kabla ya kushambuliwa (preemptive self-defense).

2. Kuchochea Chuki ya Kidini na Hatari ya Machafuko:

Vitisho hivi ni mfano wa wazi wa uchochezi wa chuki ya kidini, vinajeruhi hisia za kidini za wananchi wa Iran, watu wa eneo hili, na wote wanaotafuta haki na heshima duniani. Kuna hatari kubwa ya kuchochea mlipuko wa matukio yasiyoweza kudhibitiwa katika eneo na hata kimataifa.

3. Wito kwa Jumuiya ya Kimataifa:

Tunatarajia viongozi wa dini wa kimataifa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, na taasisi husika za kimataifa wachukue msimamo wa wazi, wa haraka na wenye ufanisi dhidi ya tishio hili la wazi na lisilo na mfano. Lazima wawazuie wale wanaojaribu kueneza vitendo vya kidhalimu, visivyo halali na vya uhalifu nje ya mipaka ya sheria za kimataifa.

Waliotia saini tamko hili ni:

Askofu Nersay Benyamin – Askofu wa Kanisa la Mashariki la Ashuru (Iran, Armenia na Georgia)

Varouj Avanessian – Mwenyekiti wa Baraza la Kiongozi wa Waarmenia wa Tehran na Kaskazini

Rabi Younes Hamami Lalehzar – Kiongozi wa jamii ya Wayahudi wa Iran

Mobed Mehraban Pouladi – Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazoroastria wa Iran

Genzora Najat Cheheili – Kiongozi wa dini wa Wamandaean (Sabean Mandaeans) wa Iran

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha