Ijumaa 13 Juni 2025 - 14:42
Taarifa ya Kituo cha Usimamizi wa Hawza kuhusu jinai iliyofanywa na utawala wa Kizayuni / Adhabu ya maangamizi inawasubiri Wazayuni

Hawza/ Kituo cha Usimamizi wa Hawza, sambamba na kulaani uvamizi wa jinai za utawala wa Kizayuni na kutangaza kuunga mkono vikosi vya kijeshi katika kuuadhibu kwa ukali na kwa maangamizi utawala huo wa waporaji, kinatoa mkono wa pole kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, kwa wanazuoni wakuu (marāji‘ taqlīd) na kwa wananchi wote adhimu wa Iran kwa kupata shahada kundi la wananchi wenzetu, makamanda wa jeshi na wanasayansi wa nyuklia.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, ifuatayo ni matini kamili ya taarifa ya Kituo cha Usimamizi wa Hawza, kwa mnasaba wa uvamizi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya nch ya Iranii:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

".إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِینَ مُنْتَقِمُون"

Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu.

Shambulizi la kinyonge na la kinyama la utawala wa jinai wa Kizayuni, lililotekelezwa kwa misingi ya kukata tamaa na kushindwa, limeonesha wazi kuwa utawala huu unao uwa watoto ambao umekuwa na ujasiri wa kupindukia kutokana na silaha za nchi za Magharibi na msaada kamili wa serikali ya Marekani, umefikia kilele cha jinai dhidi ya watu wa eneo hili na sasa umekaribia mwisho wa maisha yake ya fedheha.

Tayari ilishatabiriwa kuwa kushindwa kwa fedheha hivi karibuni kwa utawala huu katika uwanja wa kijasusi dhidi ya maafisa waaminifu wa taasisi za kiintelijensia za Jamhuri ya Kiislamu, kutawaingiza kwenye hali ya kuchanganyikiwa kiasi cha kuvuruga mfumo wao wa kufanya maamuzi.

Kituo cha Usimamizi wa Hawza, sambamba na kulaani uvamizi huu wa jinai na kutangaza kuunga mkono vikosi vya kijeshi katika kuwaadhibu kwa vikali na kuuangamiza utawala huu dhalimu, kinatoa mkono wa pole kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, kwa Mar'ajii idham, na kwa wananchi wote adhimu wa Iran kwa kupata shahada kundi la wananchi wenzetu, makamanda wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia.

Kituo cha Usimamizi wa Hawza

23 Khordad 1404.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha