Jumamosi 14 Juni 2025 - 21:17
Iran ni nchi pekee ya Kiislamu iliyosimama kwa ujasiri dhidi ya Marekani na Israel

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Kalb Jawad Naqawi, Imamu wa Ijumaa wa Lucknow, huku akilaani vikali shambulio la Wazayuni dhidi ya Iran, alisisitiza kuwa Iran ndiyo nchi pekee ya Kiislamu inayosimama kwa ujasiri dhidi ya Marekani na Israel.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Kalb Jawad Naqawi, Imamu wa Ijumaa wa mji wa Lucknow na Katibu Mkuu wa Baraza la Maulamaa wa India, katika kujibu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alitaja hatua hiyo kuwa ni sawa na kuwashwa kwa moto wa Vita Kuu ya Tatu ya Dunia katika eneo hilo.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Naqawi, alisisitiza kuwa kwa sasa, ni Iran pekee ndiyo inayosimama kidete dhidi ya nchi jeuri ulimwenguni zinazoongozwa na Marekani na utawala wa Kizayuni, ilhali hakuna nchi yoyote ya Kiislamu inayothubutu hata kutamka neno moja dhidi ya nchi hizo za kibeberu. Aliongeza kuwa, ni huu upinzani wa Iran ndio ambao siku zote umekuwa ni mwiba machoni mwa mabeberu wa kikoloni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha