Jumanne 22 Julai 2025 - 04:06
Ujumbe wa Ashura utaendelea muda wa kuwa kuna dhulma, udikteta na ufisadi

Hawza / Ayatollah Sayyid Abdullah Ghuraifi, mmoja wa maulamaa mashuhuri wa Bahrain, amesisitiza kuwa ujumbe wa Ashura ni kukataa ufisadi, dhulma, uovu, upotovu, batili na utumwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyid Abdullah Ghuraifi, mmoja wa maulamaa mashuhuri wa Bahrain, katika hotuba yake aliyotoa katika Msikiti wa Imam Swadiq (as) ulioko katika eneo la "Quful" huko Manama, mji mkuu wa Bahrain, alisisitiza kuwa; ujumbe wa Ashura ni kukataa ufisadi, dhulma, uovu, upotovu, batili na utumwa.

Ayatollah Sayyid Abdullah Ghuraifi alisema kuwa ujumbe wa Ashura unabeba dhima ya islah (marekebisho): "Sikuja ila kwa ajili ya kuleta islah" hasa katika zama hizi ambazo ufisadi na dhulma vimeenea, maadili yameporomoka, malengo makuu yamekufa, upotovu umeenea na fitina zimeshika kasi.

Yeye alisisitiza juu ya ulazima wa sauti ya Ashura, sauti ya Imam Husein (as), na sauti ya islah, amr bil-ma’ruf na nahy anil-munkar, na akasema kwamba: Maadamu upotovu, dhulma na ufisadi vinameenea, na maadamu ukandamizaji na udhalimu umejaa, ni lazima Imam Husein (as) na Ashura viendelee kuwepo.

Ayatollah Ghuraifi aliongeza kuwa: Imam Husein (as) ni kielelezo cha maadili, malengo makuu na misingi, na Ashura ni kielelezo cha amani, usalama na msamaha.

Mwanazuoni huyu wa Bahrain alikataa kauli zinazodai kuwa “Ashura ya Husein” ni tukio la kihistoria lililopita, na akasisitiza umuhimu wa kukumbuka uelewa, vigezo na ujumbe wa Ashura katika zama hizi kwa ajili ya kukabiliana na kuongezeka kwa matatizo na wasiwasi katika zama hizi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha