Jumatatu 21 Julai 2025 - 04:50
Kumtaja Imam Husein (as) ni nuru ya muongozo wa maisha na ni andao bora kabisa kwa ajili ya Akhera

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Ahmad Ali Abidi, katika hotuba zake alisisitiza juu ya thamani ya kiroho ya majlisi za maombolezo na kumbukumbu ya Imam Husein (as), na akasema kwamba kumtaja Imam Husein (as) si tu kwamba kunang’arisha njia ya maisha, bali pia ni andao bora kabisa kwa ajili ya akhera.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Ahmad Ali Abidi, katika khutba za Swala ya Ijumaa zilizofanyika katika Msikiti Mkuu wa Khoja mjini Mumbai, India, alisisitiza juu ya thamani ya kiroho ya majlisi za maombolezo na kumbukumbu ya Imam Husein (as), na akasema kuwa kumtaja Sayyid al-Shuhadaa Imam Husein (as) si tu kwamba kunang’arisha njia ya maisha, bali pia ni andao bora kabisa kwa ajili ya nyumba ya akhera.

Akiendelea, kwa kunukuu nafasi ya kiroho na umuhimu wa majlisi za maombolezo, alisema kuwa: “Kumtaja Imam Husein (as) si desturi ya kidini pekee, bali ni nuru inayomulika njia ya maisha ya mwanadamu na kumwelekeza kwenye ukamilifu na ukaribu kwa Mwenyezi Mungu. Kumbukumbu hii ni rasilimali bora kabisa ambayo mwanadamu anaweza kujiwekea kwa ajili ya akhera yake.”

Imam wa Ijumaa wa Mumbai aliendelea kwa kunukuu hadithi ndefu kutoka kwa Mtume Mtukufu (saw) na kuongeza kuwa: “Kwa mujibu wa riwaya hii, mambo kama vile: kusengenya, mapenzi ya dunia, kiburi, kujiona bora, husuda, ususuavu wa moyo, na kutokuwepo kwa ikhlasi katika nia, ni miongoni mwa vikwazo vikuu vya kukubaliwa kwa matendo.”

Kwa kusisitiza juu ya umuhimu wa ikhlasi katika matendo, alinukuu maneno ya Imam Khomeini (rahimahullah) na kusema: “Imam Khomeini (ra) alikuwa akisema: ‘Kama tendo halifanywi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi kutarajia kukubaliwa kwake kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni bure, tunaweza tukawadanganya watu wengine, lakini Mwenyezi Mungu anajua vilivyo katika nia zetu, na hakuna kilicho fichikana mbele Yake.’”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha