Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Ofisi ya Hadhrat Ayatollah Sistani, katika ujumbe wake, imelaani vikali uvamizi wa Israel dhidi ya Iran na kuwaua kishahidi kundi la wanazuoni, makamanda, na raia wasio na hatia.
Matini ya ujumbe ni kama ifuatavyo:
Bismillāhir-Rahmānir-Rahīm
Jinai ya alfajiri ya Ijumaa iliyofanywa na utawala ulio ivamia Palestina kwa kuwaua kishahidi kundi la wanazuoni, makamanda wa kijeshi na raia wasio na hatia wa Iran, wakiwemo wanawake na watoto, pamoja na kushambulia taasisi na vituo vya kielimu vya nchi hii, kwa mara nyingine imedhihirisha wazi ukweli wa hatari na wa uadui wa utawala huu.
Sambamba na kuomba rehema na daraja za juu kwa mashahidi wakubwa, kutoa rambirambi kwa familia zao tukufu, na kuwatakia wapone haraka waliojeruhiwa na walioathirika; tunalaani vikali tendo hili la jinai, na tunatarajia kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kuushinikiza utawala huu wa kivamizi na waungaji mkono wake, wawawekee vizuizi dhidi ya kuendeleza mashambulizi ya aina hii.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aendeleze izza na utukufu wa taifa tukufu la Iran.
Wa lā ḥawla wa lā quwwata illā billāhil-‘Aliyyil-‘Aẓīm
16 Dhul-Hijjah 1446 H.Q
Ofisi ya Hadhrat Sistani - Najaf Ashraf
Maoni yako