Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa Hadhrat Ayatollah Makarem Shirazi kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni na kuuawa kishahidi kundi la wananchi watukufu na makamanda wa kijeshi wa Iran ni kama ifuatavyo:
Bismillāhir-Raḥmānir-Raḥīm
Mashambulizi ya kinyama yaloyofanywa na utawala wa Kizayuni wenye kumwaga damu dhidi ya ardhi ya Iran, na kuuawa kishahidi kwa dhulma kundi la wanawake, watoto, wananchi watukufu, makamanda na wanazuoni wa nyuklia, yamezua wimbi la huzuni na hasira ndani ya taifa kubwa la Iran.
Bila shaka yoyote, ahadi ya Mwenyezi Mungu kuhusu kuangamia kwa madhalimu itatimia, na hivi karibuni, kwa irada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa mikono ya waumini, waraka wa mwisho wa huu mzizi wa ufisadi na waungaji mkono wake wa kimataifa utafungwa.
Katika hali hii nyeti na ya hatari, jambo linalowajibika kwa kila mmoja ni kudumisha mshikamano wa nyoyo, umoja wa maneno, na kujiepusha na matamshi na migongano inayosababisha kulegea kwa dhamira, kutikisika kwa mioyo, na kutokea kwa mfarakano na kudhoofika kwa safu za waumini.
Bila shaka yoyote, uungaji mkono wananchi kwa ufahamu na kwa uthabiti juu ya maamuzi yaliyofanywa na viongozi wa juu na majeshi, sambamba na kutojali visingizio vya wanafiki, mahasidi na wachochezi, ndio njia bora kabisa ya kukabiliana na mashambulizi ya kina ya maadui wa Uislamu.
Katika fursa ya kukaribia Siku ya Ghadir na ya wilaya ya Mtukufu Amirul-Mu’minin Ali (as), tunamuelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa dua kwa unyenyekevu, na tunamfanya yeye kuwa ni mwombezi wetu. Tuna yakini kamili juu ya ahadi ya msaada wa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa amesema:
«وَلَيَنْصُرَنَّ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ»Na hakika Mwenyezi Mungu atamnusuru yule anayemnusuru Yeye.
Wassalāmu ʿalaykum wa raḥmatullāh
Qum – Nāṣir Makārem Shīrāzī
23/3/1404
Maoni yako