Ijumaa 13 Juni 2025 - 14:46
Umoja na mshikamano chini ya mhimili wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ni jambo la lazima na la dharura

Hawza/ Hadhrat Ayatollah Nouri Hamedani amesisitiza kuwa: Katika nyakati hizi nyeti za kihistoria, umoja na mshikamano chini ya mhimili wa Waliyyul-Faqih, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, ni jambo la lazima na la dharura.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa Hadhrat Ayatollah Nouri Hamedani, kufuatia jinai ya alfajiri ya leo ya utawala wa Kizayuni ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Uvamizi wa kinyama ulio fanywa na utawala dhalimu na batili wa Kizayuni unalaaniwa vikali, na bila shaka vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vitatoa jibu la dhati dhidi ya jinai hii.

Kuuawa kishahidi idadi ya makamanda wapendwa, hasa mashahidi Bāqeri na Salāmi, pamoja na wanasayansi wa heshima wa nchi yetu – ambao inshaAllah njia yao itaendelezwa kwa nguvu na uimara na wenz wao – na pia kuuawa kwa wananchi wasio na hatia, vyote hivi vinaonesha kuwa utawala huu dhalimu, kwa ajili ya kubakia katika siku zake za mwisho, hauachi kufanya jinai yoyote ile.

Katika nyakati hizi nyeti za kihistoria, umoja na mshikamano chini ya mhimili wa Waliyyul-Faqih, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, ni jambo la lazima na la dharura, na aina yoyote ya kuibua mifarakano na migawanyiko katika jamii – kwa namna yoyote ile na kutoka kwa mtu yeyote, harakati yoyote au kundi lolote – huhesabiwa kuwa ni aina ya kushirikiana na adui. Watu wote wanapaswa kuwa macho dhidi ya hila na vitimbi vya maadui waliokula kiapo dhidi ya Uislamu na Mapinduzi, wakiongozwa na Marekani, Wazayuni na vibaraka wao.

Mwishoni, sambamba na kutoa mkono wa pole na kuomba daraja za juu kwa mashahidi wapendwa, ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape afueni majeruhi, awape ushindi wapiganaji wa Uislamu, na auangamize utawala batili wa Kizayuni.

Hussein Nouri Hamedani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha