Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, kampeni hii imeanzishwa kwa kuratibiwa na mashirika ya haki za binadamu, na hadi sasa takribani programu 7000 za kiutendaji zimepangwa kwa mujibu wa malengo ya kampeni hiyo.
Wajitolea kushiriki katika kampeni hii wamesajiliwa kwa mujibu wa vigezo vya umri, hali ya afya na ujuzi wa kiufundi (lajistiki).
Watu mashuhuri waliojitokeza kushiriki katika kampeni hii waliwahimiza wananchi kuikaribisha kwa ari na kushiriki kwa wingi, ili kutimiza wajibu wao wa kimaadili na kisiasa. Hili ni jambo la muda mrefu katika historia ya Tunisia ambapo wananchi hufikisha ujumbe wao wa mshikamano kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa kwa njia ya michezo kama soka.
Katika mkusanyiko huo, hadhira walipaza kauli mbiu isemayo: “Wakati dunia inanyamaza, ni wajibu wetu kupaza sauti!”
Makundi yenye ushawishi mkubwa kutoka nchini Libya pia, kwa kupitia tamko la pamoja, yaliungana na wenzao wa Tunisia na kuipokea kwa furaha hatua hiyo ya kiuanzilishi. Vyama vikuu vya Tunisia kama vile wawakilishi wa jamii ya wafanyakazi, wakulima, madaktari, mashabiki wa soka na hata wanamichezo wa fani nyingine walitangaza kuunga mkono kampeni hiyo.
Vikundi hivi vyote kwa sasa vimekusanyika chini ya kauli mbiu moja:
“Vizuizi lazima viondoshwe!”
Pamoja na vitisho vya wazi kutoka katika utawala wa Israel unaoua watoto, dhidi ya mkusanyiko huu mkubwa, waandaaji wa kampeni hiyo wamesisitiza kuwa wanaazimia kuendelea na njia hiyo. Msemaji wa kampeni hiyo, "Waleh Nawwar", alisema:
“Hakuna lisilowezekana kwetu.”
Maoni yako