Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sheikh Ali al-Khatib, Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kishia nchini Lebanon, alimpokea Balozi wa Iran nchini humo, Mujtaba Amani, pamoja na Sayyid Ali Khomeini, katika makao makuu ya Baraza hilo katika eneo la al-Hazmiyyeh. Washiriki walimkumbuka Imam Khomeini kwa heshima katika kumbukizi ya kufariki kwake, na wakazungumza kuhusu sifa zake za kibinafsi, nafasi ya kiuongozi huyo, na mapinduzi aliyoyaongoza.
Sheikh al-Khatib alisema: Tumempoteza Imam Khomeini, ambaye haiba yake iliambatana na ujasiri na kujitolea, na nuru yake iliangaza kote duniani.
Aliongeza kusema: Maisha yake yalijaa ukarimu na mafanikio yaliyowekwa wakfu kwa masuala ya Umma na mataifa yake. Imam Khomeini alianzisha harakati kubwa zaidi ya mapinduzi ambayo mafundisho yake yalichukuliwa kutoka katika roho ya Uislamu.
Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kishia nchini Lebanon alisema: Kiongozi huyo mkubwa wa mapinduzi ya Kiislamu, katika mapinduzi yake yenye baraka, alipambana na dhulma na udikteta duniani, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, licha ya kuwekewa vizuizi na vikwazo, imesimama imara katika utiifu kwa njia ya Imam Khomeini (r.h) kwa kuendelea kuiunga mkono jamii ya wanyonge na malengo ya haki ya Umma.
Sheikh al-Khatib aliendelea kusema: Miongoni mwa malengo haya, suala la Palestina limo kileleni, sambamba na kuunga mkono wananchi wa Lebanon katika mapambano yao dhidi ya uvamizi na uporaji wa Kizayuni ambao umehusika na mauaji ya halaiki ya watoto, wanawake, na wazee wasio na ulinzi, huku ukikiuka kwa uzito mikataba yote pamoja na thamani za kidini na kibinadamu—jambo ambalo linathibitisha kauli ya Imam Khomeini (r.h) aliposema kuwa "Israel ni uvimbe wa saratani unaopaswa kung’olewa kabisa".
Maoni yako