Alhamisi 5 Juni 2025 - 17:25
Raj‘a: Moja ya Imani Thabiti za Kishia

Hawza/ Ingawa mahali halisi pa malipo na adhabu za wanadamu ni ulimwengu wa Akhera, lakini Mwenyezi Mungu ameazimia kutekeleza sehemu ya malipo na adhabu hizo hapa hapa duniani.

Shirika la Habari la Hawza - Moja ya matukio muhimu yatakayotokea wakati wa kudhihiri Imam Mahdi (as) ni suala la "raj‘a" (kurejea kwa wema na waovu duniani), ambalo ni miongoni mwa imani thabiti za Kishia.

Maana ya Raj‘a

Neno "raj‘a" kwa lugha ya kawaida inamaanisha “kurejea.” Katika fasihi ya kidini, "raj‘a" ni kurejea kwa hoja wa Mwenyezi Mungu na Maimamu watoharifu (as), pamoja na kundi la waumini waaminifu na makafiri na wanafiki, katika ulimwengu huu wa kidunia; yaani, kwa amri ya Mwenyezi Mungu, wao watahuishwa tena na kurejea duniani. Tukio hili ni mfano wa ufufuko mkuu (Kiyama), lakini hutokea kabla ya Siku ya Kiyama hapa duniani.

Falsafa ya Raj‘a
Ingawa sehemu ya msingi ya malipo na adhabu kwa wanadamu ni ulimwengu wa Akhera, lakini Mwenyezi Mungu amependa kutekeleza sehemu ya malipo na adhabu hizo hapa duniani.

Imam Baqir (as) anasema katika muktadha huu:

«... أَمَّا اَلْمُؤْمِنُونَ فَیُنْشَرُونَ إِلَی قُرَّةِ أَعْیُنِهِمْ وَ أَمَّا اَلْفُجَّارُ فَیُنْشَرُونَ إِلَی خِزْیِ اَللَّهِ إِیَّاهُمْ ...»

“Ama waumini hufufuliwa ili waione furaha ya macho yao, na ama waovu hufufuliwa ili waone fedheha ya Mwenyezi Mungu kwao.” (Biharul An-war, juzuu ya 53, uk. 64)

Waumini hurudi duniani ili wapate heshima na macho yao yakiwa yameridhika, na waovu hurudi ili Mwenyezi Mungu awadhilishe.

Lengo jingine la "raj‘a" ni kuwapa waumini fursa ya kupata sa‘ada ya kumnusuru Imam wa Zama (as).

Kwa mfano, katika mojawapo ya ziyara kwa Imam wa Zama (as), tunamwambia maneno haya:

«... مَوْلاَیَ فَإِنْ أَدْرَکَنِیَ اَلْمَوْتُ قَبْلَ ظُهُورِکَ فَإِنِّی أَتَوَسَّلُ بِکَ وَ بِآبَائِکَ اَلطَّاهِرِینَ إِلَی اَللَّهِ تَعَالَی وَ أَسْأَلُهُ أَنْ یُصَلِّیَ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ وَ أَنْ یَجْعَلَ لِی کَرَّةً فِی ظُهُورِکَ وَ رَجْعَةً فِی أَیَّامِکَ لِأَبْلُغَ مِنْ طَاعَتِکَ مُرَادِی وَ أَشْفِیَ مِنْ أَعْدَائِکَ فُؤَادِی ...»

“Ewe Mola wangu! Ikiwa mauti yatanifikia kabla ya kudhihiri kwako, basi kwa kupitia kwako na kwa baba zako watoharifu namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, na namwomba amuombee rehma Muhammad na Ahli wa Muhammad, na aniwekee mimi kurejea wakati wa kudhihiri kwako na kurejea katika siku zako ili nipate kutimiza lengo langu la kukutii na niponye kifua changu dhidi ya maadui zako.” (Biharul-anwar, juzuu ya 99, uk. 116)

Nafasi ya Raj‘a
Raj‘a ni moja ya imani za hakika katika madhehebu ya Kishia, ambayo ina mashiko ya msingi katika makumi ya aya za Qur'ani na mamia ya hadithi kutoka kwa Mtume Mtukufu (saw) na Maimamu watoharifu (as).

Muhaddith mashuhuri, marehemu Sheikh Hurr al-‘Amilī, mwishoni mwa kitabu chake “الإیقاظُ مِن الهَجعَة بالبُرهان عَلی الرَّجعَة” anaandika:

«فقد ذکرنا فی هذه الرسالة من الأحادیث والآیات والأدلّة ما یزید علی ستمائة وعشرین ولا أظنّ شیئاً من مسائل الاُصول والفروع یوجد فیه من النصوص أکثر من هذه المسألة.»

“Hakika tumetaja katika risala hii zaidi ya hadithi, aya na hoja 620 kuhusu "raj‘a", na sidhani kuwa kuna suala lolote katika masuala ya msingi au matawi ya dini ambalo lina ushahidi mwingi kama suala hili.”

Utafiti huu unaendelea...

Imenukuliwa kutoka kitabu cha “Negin-e Āfarinish” huku ikifanyiwa marekebisho

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha