Jumanne 3 Juni 2025 - 17:59
Dunia haisikii sauti ya wazazi waliopoteza watoto wao huko Ghaza

Hawza/ Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Wazazi, amependekeza siku hii ipewe jina la wazazi wa watoto walio dhulumiwa wa Palestina.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Wazazi, katika ujumbe wake amependekeza siku hii iitwe kwa jina la "wazazi wa watoto walio dhulumiwa wa Palestina".

Katika ujumbe huo imeelezwa kuwa: Wazazi katika kila jamii wana nafasi muhimu katika malezi na uundwaji wa kizazi kijacho, na kuheshimu baba na mama kwa mtazamo wa kidini, kijamii na kisheria kuna umuhimu mkubwa. Lakini swali ni hili: Kwa nini dunia haizingatii mateso na huzuni za wazazi walio dhulumiwa wa Palestina?

Akiashiria kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Wazazi yenye kichwa kisemach: “Malezi na Makuzi ya Wazazi”, amesisitiza kuwa: Wakati dunia inazungumzia malezi ya familia, huko Ghaza na Palestina misingi ya familia imefutika kabisa. Nyumba zimebomolewa, wazazi wanaomboleza watoto wao, na watoto wamesalia bila hifadhi. Je, si wakati umefika sasa siku hii ya kimataifa iitwe kwa jina la wazazi wa watoto wa Palestina?

Tuna mashahidi wa kina mama huko Ghaza ambao baada ya kuuawa mashahidi watoto wao, bado wanaendelea kuwahudumia waliojeruhiwa. Wazazi wa hawa watoto hawa ni alama ya dhulma katika dunia inayodai haki na amani, lakini imebakia kimya mbele ya jinai hizi.

Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan pia ameongeza kuwa: Malezi na ulinzi wa watoto ni jukumu kuu la familia. Watoto wanahitaji mazingira yaliyojaa mapenzi na usalama ili wakue na kupata utulivu. Lakini katika ardhi ya Palestina kama Gaza na Rafah, mazingira haya yameangamizwa kabisa. Jumuiya ya kimataifa kwa nini inanyamaza kimya mbele ya hali hii ya kutisha?

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha