kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Wananchi waliopo jijini Nairobi Nchini Kenya, waliunganaga na baadhi ya wairani wanaoishi nchini humo kwa ajili ya kuadhimisha miaka 36 tangia kufariki kwa Kiongozi mwanzilishi wa Serekali ya Mapinduzi ya Irani Imam Khomeini (ra), katika hafla hiyo ambayo iliongozwa na Balozi wa Irani nchini kenya Dkt. Ali Gholampour, umati mkubwa uliweza kujitokeza kwa ajili ya kumuenzi Imam Khomeini (ra), pamoja na kuelezea mchango wake alio uonesha katika huu ulimwengu, ikiwa ni pamoja na kuwatetea wanyonge wote waliopo ulimwenguni hapa hasa hasa akitilia mkazo kadhia ya palestina.
Balozi wa Irani nchini Kenya Dkt. Ali Gholampour, alikuwa ni miongoni mwa watu ambao waliweza kuelezea kwa kina zaidi wasifu wa Imam Khomeini (ra), vilvile ukiachilia mbali hotuba yake adhim, wapo wahadhiri wengine mashuhuri ambao nao pia walipata nafasi ya kuzungumza katika hafla hiyo, akiwepo Hujatul-Islam Sheikh Ali Samoja, ambae nae pia aliweza kuelezea mambo mengi ambayo yalikuwa yanahusiana na Imaam Khomein (ra).
Maoni yako