Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Papa amesema: Usitishaji mapigano unapaswa kuanza sasa hivi ndani ya Ghaza! Vilevile, wafungwa wote wanapaswa kuachiliwa huru kwa kuzingatia sheria zote za kibinadamu.
Papa ameongeza kuwa: Leo, kutoka Ukanda wa Ghaza, tunasikia vilio vya kina mama na kina baba wanaowakumbatia miili ya watoto wao waliopoteza maisha. Watu hawa wanalazimika kutoka katika maeneo ya hifadhi – ambayo huenda ni salama zaidi kiasi – ili kupata maji na chakula kidogo.
Papa alitoa hotuba hii siku ya Jumatano, ikiwa ni siku moja tu baada ya takriban watu 50 kuuawa kishahidi na kujeruhiwa huko Ghaza wakati wakijaribu kupata msaada wa chakula katika maeneo ya ugawaji misaada, na akatoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja.
Maoni yako