Jumapili 25 Mei 2025 - 23:34
Viongozi na Taasisi za Kiislamu Uingereza Wamemtaka Waziri Mkuu Kusitisha Mazungumzo ya Kibiashara na Israel

Hawzah/ Viongozi na taasisi za Kiislamu nchini Uingereza wametaka kusitishwa kwa mazungumzo ya kibiashara kati ya Uingereza na Israel, na katika barua ya pamoja kwa Waziri Mkuu, wameelezea hali ilivyo sasa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, makumi ya vituo vya Kiislamu nchini Uingereza, ikiwemo misikiti, waliandika barua ya pamoja kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo wakitaka mazungumzo ya kibiashara na Israel yasitishwe haraka iwezekanavyo; miongoni mwa madai mengine yao ni kuchukuliwa hatua za haraka na zenye nguvu zaidi kuhusiana suala la Palestina.

Viongozi na taasisi za Kiislamu nchini Uingereza, zikiwemo Taasisi ya Msikiti Mkuu wa London, Chuo cha Kiislamu cha Manchester, na Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini Uingereza, wamesema kuwa "kasi ya kuchukua hatua zinazohitajika ili kukabiliana na uhalifu wa Israel ni ndogo sana."

Katika barua hiyo imeandikwa:
"Kwa zaidi ya miezi kumi na nane, tumekuwa tukishuhudia matukio ya kusikitisha ya uharibifu usiovumilika wa utu wa binadamu huko Gaza. Tumeona jinsi Israel, kinyume na sheria zote za kimataifa za kibinadamu, ilivyotumia njaa kama silaha dhidi ya raia wasio na ulinzi."

Wametoa wito kwa serikali kuzingatia mambo manne muhimu katika hatua zake za msingi:

1- Kurejesha makubaliano ya kusitisha mapigano,
2- Kukomesha haraka iwezekanavyo vikwazo kwa Ghaza,
3- Kuidiriki hali ya sasa inayo wakabilli wapalestina,
4- Na kusitisha uuzaji wa silaha, kwani ni kinyume cha sheria za kimataifa.

Katika tamko hilo wamesema: "Tuna wasiwasi mkubwa kwamba Serikali ya Uingereza haito chukua hatua yeyote katika hali hii ya dharura."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha