Jumamosi 17 Mei 2025 - 20:35
Rais wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan: Ukombozi wa Quds ni ahadi ya Mwenyezi Mungu

Hawza/ Katika kumbukumbu ya siku ya kukaliwa kimabavu kwa mji mtakatifu wa Quds, Seneta Raja Nasir Abbas Jafari, katika tamko alilolitoa, amelaani jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa ukombozi wa Quds na ushindi wa taifa lenye kudhukumiwa la Palestina ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ambayo bila shaka itatimia.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya  Shirika la Habari la Hawza, kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya siku ya kukaliwa kwa mabavu mji mtakatifu wa Quds, Seneta Raja Nasir Abbas Jafari, Rais wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan, katika tamko alilolitoa huku akilaani jinai za utawala wa Kizayuni, amesisitiza kwamba ukombozi wa Quds Tukufu na ushindi wa taifa lenye kudhulumiwa la Palestina ni ahadi ya Mwenyezi Mungu isiyo na shaka ambayo hakika itatimia.

Ameongeza kusema: “Kwa imani kamili na yakini ya moyoni, tunaamini kuwa hatimaye siku itawadia ambapo dunia itaokolewa kutoka katika makucha ya dhulma, uvamizi na ubaguzi, na itasalia katika kivuli cha uadilifu, uhuru na utu wa kibinadamu. Taifa lenye kudhulumiwa la Palestina ambalo kwa miaka mingi limekuwa likiandamwa na ukaliaji wa mabavu, uvamizi na kuzingirwa kidhalimu, bila shaka litaushuhudia uhuru wa kweli. Wakati dhulma itakapokoma, jua la haki litang’aa kwa mwangaza wa ajabu kuliko wakati wowote ule.”

Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Pakistan ameongeza kusema: “Mzozo wa Palestina si tu mzozo wa kisiasa au wa mipaka, bali ni mapambano ya kihistoria kati ya uwanja wa haki na batili; ni mapambano kati ya wanyonge dhidi ya mababe wa kibeberu, na msimamo wa kupinga ukaliaji wa mabavu na dhulma. Mapambano haya ni mtihani mkubwa wa ubinadamu, na tunaamini kwamba katika mapambano haya, ushindi wa mwisho utakuwa wa taifa linalostahamili la Palestina na wa mataifa yote yanayopigania uhuru.”

Amesisitiza: “Siku itawadia ambapo sauti ya adhana itasikika kutoka kwenye minara ya Msikiti wa Al-Aqsa uliokuwa huru, watoto wa Kipalestina badala ya kusikia milipuko na ving’ora vya hatari, wataenda shule huku wakiwa na tabasamu na utulivu, na kina mama wa Kipalestina watawabeba watoto wao kwa usalama katika vifua vyao. Hii ni ahadi ambayo si tu watu huru wa dunia bali hata Mwenyezi Mungu Mtukufu ameahidi kutimia kwake.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha