Ijumaa 16 Mei 2025 - 11:06
Njaa na ukame huko Ghaza ni ishara ya ukosefu wa maadili ya kibinadamu duniani

Hawza/ Mgogoro wa Ghaza ni janga la kibinadamu ambalo athari zake mbaya zinawakumba watu wa tabaka lote, lakini mzigo mkubwa zaidi unabebwa na watoto. Mzigo huu unavunja mifupa yao, kwa hakika, zaidi ya watoto 60,000 wanateseka kwa utapiamlo wa kiwango cha juu mno, na maelfu yao wanakumbwa na mauti.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha Tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza, takriban miezi miwili baada ya utawala wa Kizayuni kukiuka makubaliano ya usitishaji vita, utawala huu wa kiuaji ulianzisha vizuizi vya kipekee na vya kinyama dhidi ya Ghaza, na ulifunga kabisa njia zote za mipakani kwa misaada ya kibinadamu, kama vile: maji, chakula, mafuta na dawa.

Kwa mujibu wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP), hifadhi zote za chakula huko Ghaza zilimalizika mwezi Aprili 2024, na hali hiyo tangu mwezi Machi ilikuwa tayari imegeuka kuwa janga. Hata majiko yaliyo fadhiliwa kutoa misaada, ambayo kwa wastani yalikuwa yakipika zaidi ya milo milioni moja kwa siku, hayana chakula tena. Na vyakula vilivyobakia vimepanda bei kwa asilimia "1400", hali ambayo imenifanya ununuzi wake kuwa jambo lisilowezekana kabisa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha