Jumatatu 28 Aprili 2025 - 19:57
Maandamano Makubwa yafanyika katika Miji ya Marekani yakilenga Kusitishwa Mara Moja vita vinavyo endelea huko Ghaza

Maandamano makubwa yamefanyika siku ya Ijumaa katika miji kadhaa nchini Marekani huku yakihudhuriwa na watu wengi, watu hao walidai kusitishwa mara moja kwa vita huko Ghaza na kusema kuwa njia za mipakani za Ghaza lazima zifunguliwe ili misaada ya kibinadamu iweze kuwafikia watu wenye njaa.

Shirika la Habari la Hawza- kwa mujibu wa taarifa ya Kituo cha Habari cha Palestina, mamia ya waandamanaji waliokusanyika katika uwanja wa Herald, jijini New York, walilaani vitendo vinavyo fanywa na utawala wa Kizayuni na walitaka kusitishwa vita visivyo na usawa huko Ghaza.

Matakwa mengine ya waandamanaji hao yalikuwa ni kuiwekea vikwazo Israel, kutouza silaha kwa utawala huo unao mwaga damu, na kukabidhi misaada ya kibinadamu haraka kwa watu wa Ghaza.

Waandamanaji wa Marekani walionyesha kutoridhika na walionesha chuki dhidi ya matumizi ya fedha za kodi wanazo zitoa katika vita dhidi ya Ghaza na katika kuwaua raia wasio na hatia.

Maandamano kama hayo pia yalifanyika katika miji ya Washington, Milwaukee, Dallas, San Francisco na Chicago, yakiwa na kaulimbiu na ujumbe huu huu, kama sehemu ya shughuli za vikundi hivi kwa ajili ya "Siku ya Kimataifa ya kujitolea kwa ajili ya watu waliodhulumiwa wa Ghaza."

Waandamanaji walitaka kufunguliwa tena mipaka ya Gaza na kukabidhiwa haraka misaada yote ya kibinadamu kwa watu na wakazi wa eneo hilo.

Kwa shinikizo kutoka kwa taasisi za kiraia na wanafunzi wanaoiunga mkono Palestina, Taasisi ya Teknelojia ya Chuo Kikuu cha Massachusetts (MIT) ilifanikiwa kuivunja moja ya kampuni kubwa zaidi inayo tengeneza silaha za Israel.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha