Shirika la Habari la Hawza- waziri mkuu wa Ufaransa, François Baroin, amelaani vikali tukio la kupigwa na kuuawa kwa mwislamu mmoja ndani ya msikiti. Kwa masikitiko, tukio hili lilisababisha kifo cha mwislamu aliyeshambuliwa kwa kisu.
Kwa mujibu wa taarifa ya "France 24", polisi wa Ufaransa walifanikiwa kumtia mbaroni muuaji huyo, ambaye alirekodi video ya kitendo chake cha kikatili na kuisambaza.
Ripoti zinaonyesha kuwa muuaji alimchoma kwa kisu mtu alie kuwa akiswali mara kadhaa kisha akaanza kurekodi video. Uhalifu huu wa kusikitisha ulitokea Ijumaa katika msikiti wa kijiji cha Land Kamp, katika eneo la Gard kusini mwa Ufaransa.
Ingawa Baroin aliandika: "Tunaungana kwa dhati na familia ya marehemu na Waislamu wote ambao wameshtushwa sana. Hakikisheni kwamba serikali itamkamata na kumwadhibu muuaji huyu," lakini Waislamu wa Ufaransa wanaamini kwamba chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) nchini humo inazidi kuongezeka.
Mapema sikubya Jumamosi, wachunguzi wa kesi hii walitangaza kwamba mauaji haya yalifanywa kwa misingi ya chuki dhidi ya Uislamu katika nchi hiyo.
Video zilizorekodiwa zinathibitisha jambo hili wazi wazi, kwani muuaji, alipokuwa akirekodi, alitoa matusi dhidi ya Uislamu na kulitaja jina la Mungu kwa tafsiri ya Kiarabu kisha kulitukana.
Kwa mujibu wa ripoti, mtu aliye uliwa alikuwa ni kijana wa kijiji hicho hicho, ambaye alikuwa anafahamika kwa sifa njema miongoni mwa wakazi wa Land Kamp, jambo lililofanya mauaji yake yawahuzunishe watu wengi mno.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Bruno Retailleau, siku ya tukio hilo, alitoa ujumbe wa kulielezea tukio hili na kusema ni tukio la kinyama.
Maoni yako