Jumatano 23 Aprili 2025 - 16:33
Matumizi ya akili mnemba ni jambo la wajibu / Mafaqihi wabainishe hukumu za kifiqhi zinazohusiana na akili mnemba

Mjumbe wa Jumuiya ya walimu wa Hawza ya Qom {Jamiat Mudarrisin} alieleza wazi kwamba: Kuwekeza nguvu katika mkakati mara nyingi kunahusiana na mienendo ya kawaida, na akili mnemba pia ina nafasi iliyo dhahiri na muhimu katika uwanja huu. Kwa hivyo, ni wajibu kwa dola kutumia uwezo wake wote katika nyanja hii, wanazuoni wa fiqih pia wana jukumu la kuonesha bidii katika kubainisha hukumu za kifiqhi zinazohusiana na jambo hili.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa  Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Mohsen Araki katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa kitaifa wa kitaalamu kuhusu “Matumizi na Uwezo wa Akili mnemba katika Kuendeleza hatua za elimu ya Binadamu” uliofanyika Jumanne katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa Ghadir mjini Qom, alizungumzia vipengele vya kifiqhi na baadhi ya wajibu wa kisheria kuhusu matumizi ya teknolojia ya akili mnemba.

Mwanachama wa Baraza Kuu la Hawza, kwa kurejelea nafasi ya akili mnemba kama chombo kipya kilicho na nguvu, alisema: Kujihusisha na nguvu hii mpya pamoja na masuala ya kifikra na kiteknolojia yanayohusiana nayo, vilevile matumizi na shughuli zinazotegemea akili mnemba, ni miongoni mwa majukumu ya watu wote kwa ujumla na hasa ni jukumu la utawala wa Kiislamu. Hii ni kwa sababu masuala yanayohusiana na akili mnemba katika muktadha wa hukumu za kifiqhi ni sehemu ya majukumu ya jumla, na kila jukumu linalohusiana na maslahi ya kijumla ya jamii huelekezewa utawala.

Aliongeza kuwa: Kuwekeza nguvu katika mkakati mara nyingi kunahusiana na mienendo ya kawaida, na akili mnemba pia ina nafasi iliyo dhahiri na muhimu katika uwanja huu. Kwa hivyo, ni wajibu kwa dola kutumia uwezo wake wote katika nyanja hii, wanazuoni wa fiqih pia wana jukumu la kuonesha bidii katika kubainisha hukumu za kifiqhi zinazohusiana na jambo hili.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha