Shirika la Habari la Hawza, Somayeh Erdogan Bayraktar, mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Jumuiya ya Wanawake na Demokrasia, alikumbushia kuhusu madhara yanayosababishwa na kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi kati ya wanawake waumini wa dini na wanajamii wengine duniani kote, hasa katika nchi za Magharibi.
Akiwasilisha matokeo ya utafiti uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Ibn Khaldun, alielezea mwenendo wa kutisha unaoendelea na kusema: wanawake wanaozingatia hijabu ya Kiislamu mara nyingi huhisi kwamba haki zao katika nyanja mbalimbali za jamii kama elimu, ajira au shughuli za michezo zinapuuzwa. Akinukuu matukio ya hivi karibuni nchini Ufaransa, alikosoa vikali marufuku ya hijabu katika michezo kwenye nchi hiyo.
Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Jumuiya ya Wanawake na Demokrasia alisisitiza: "Sera hizi zinawazuia wanawake kuishi maisha ya kawaida katika jamii na zinatengeneza vizuizi vinavyotokana moja kwa moja na kupuuzwa kwa haki za binadamu za wanawake katika kuchagua mavazi yao."
Bi Bayraktar alikosoa vikali sera ya nchi ya Ufaransa ya kuwakataza wanawake kuvaa hijabu katika michezo na akabainisha kuwa hatua kama hizi zinaweza kupelekea kupigwa marufuku wanawake kuweza kujieleza, na kubadilisha tafsiri ya maadili ya kibinadamu kama vile utaifa, lugha na hata sifa za kimwili; hali inayogeuza maadili hayo na kuyadhalilisha. Alisema: "Kwa hakika hii siyo sekularism, bali kwa tafsiri ya ndani ni matumizi ya sekularism kama chombo cha kuchochea chuki dhidi ya Uislamu."
Aliitaka jamii kutoa jawabu la pamoja dhidi ya sera hii hasi na akatangaza kuwa sisi wanawake wa kiislamu kamwe hatutoachana na haki zetu, na tutafanya juhudi kubwa kuzihuisha haki hizi.
Maoni yako