Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza A'rafi alielezea juhudi zilizofanywa katika miaka michache iliyopita za kuanzisha masomo ya ijtihadi katika Sarf na Nahw, akasema: "Licha ya juhudi zilizofanywa, hasa kozi za kitaalamu za sarufi ya lugha ya kiarabu katika ngazi ya tatu na nne kwenye sekta maalum, bado hatujapata mafanikio yaliyokusudiwa. Ni muhimu kwamba Hawaza zielekee katika kuunda mfumo wa ijtihadi-Adabi. Kwa msingi huu, tunakaribisha masomo ya ijtihadi-Adabi yatakayozunguka kutatua mahitaji na kujibu maswali yanayohusiana na uchambuzi wa fiqh kutoka katika Qur'ani na Hadithi."
Mudiri wa Hawza aliongeza kusema: "Hawza" zinapaswa kushughulika na uzalishaji wa elimu na nadharia katika nyanja za kisarufi na lugha. Leo hii tunahitaji watu wataalamu na watafiti katika eneo hili wafanye kazi na kwa kutoa makala na tafiti za kielimu, kusaidia kuongeza ufahamu wa kielimu katika Hawza. Elimu za sarufi ni sehemu ya awali ya ijtihadi na zina athari moja kwa moja katika uchambuzi wa aya na hadithi. Ingawa kiwango cha mahitaji ya elimu za sarufi, hasa Sarf, Nahw, Lugha, Maana, Bayaan na Badi' kina tofautiana, lakini katika shule ya kidini yenye maelfu ya wanafunzi, ni lazima kuwepo na watu kadhaa ambao wataongoza katika elimu za safuri."
Mjumbe wa Baraza la Wanazuoni wa Sharia aliongeza kusema: "Uhitaji wa Sarf, Nahw na Lugha kwa ijtihadi kati ya wasomi ni jambo linalokubalika wazi. Hata hivyo, baadhi wanadhani kuwa matumizi ya maani, bayaani na badi’ yanaukomo, hivyo basi hayana nafasi kubwa katika ijtihadi. Mtazamo huu unajitokeza kwa sababu maneno ya Ma’asumīn (a.s) ni kama matini za kisheria, na maelezo ya kifasihi kama vile methali na mapambo ya kifasihi hayatumiki, wakati ambapo katika Qur'ani Tukufu na hadithi, kuna mifano mingi ambapo mafumbo ya kifasihi yamekuwa yakitumika na mara nyingine, mafumbo haya yana athari katika uchambuzi wa hukumu za kisheria. Kwa hiyo, kuna haja ya kuzingatia mafumbo haya kwa umakini zaidi. Kwa mfano, katika aya tukufu (قُوا أَنْفُسَكُمْ وَأَهْلِیکُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ), kwa kutumia neno (أهلیکم), inaweza kuhusisha watoto wa kumtunza na watoto wa mke pia."
Mudiri wa Shule za Kidini (Hawza) alielezea pia masuala mapana ya ijtihadi na kusema: "Kanuni muhimu za lugha zinahitaji kazi ya ijtihadi. Katika maana za herufi na vitendo, kuna maswali makubwa ambayo yanahitaji kujibiwa; miongoni mwa maswali hayo ni: Je, maana za herufi zipo katika surua ya kushirikiana kilafudhi au kwamba katika baadhi ya matukio zinatumika kama uhalisia na majazi? Kuzingatia masuala kama haya, sio tu kutasaidia kuongeza ufahamu wa kielimu katika Hawza, bali pia kunaweza kuwa na manufaa katika malezi ya wanafunzi na watafiti vijana."
Imam wa Ijumaa wa Qom alisisitiza: "Lazima tujitahidi kuunda mazingira bora ya tafiti na utafiti katika nyanja hizi."
Maoni yako