Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmed Al-Qattan, Rais wa Jumuiya ya "Qauluna wa Amal" na mwanazuoni wa Ahlu-Sunnah wa Lebanon, katika ibada ya kumuomboleza Imam Husein iliyofanyika nyumbani kwa Hajj Jihad Mousa katika mji wa Saadnayel, alisisitiza kuwa; sisi Lebanon muda wa kuwa tuna viongozi thabiti kama Sheikh Naeem Qasim, Katibu Mkuu wa Hezbollah, na Nabih Berri, Mwenyekiti wa Bunge pamoja na viongozi wengine wote wanaotaka kuhifadhi nguvu, heshima, na uwezo wa Lebanon katika kukabiliana na changamoto, hatuogopi.
Sheikh Al-Qattan aliendelea kusema: Tunaposema tunajihusisha na mapinduzi na kusimama kwa Imamu Hussain (a.s), tunahisi heshima, tunahisi hadhi. Tunaposema tunajihusisha na mhimili wa muqawama, tunajivunia na kuhisi heshima, tunahisi kuwa sisi ni wachache katika ardhi hii, dhidi ya wengi wanaotumia vibaya mamlaka yao na kuangamiza ubinadamu.
Maoni yako