Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Najma Salihi, mhadhiri na mtafiti wa Jamiaat al-Zahra (sa), amenakili kuwa: Ni kweli kuwa binadamu ameumbwq kwa taabu; lakini baadhi ya watu ni kama kioo cha dhahiri cha uvumilivu wa Mwenyezi Mungu duniani, na bibi Zainabu (sa) alikuwa wa aina hiyo.
Yeye aliyezaliwa katika nyumba ya Ali (a.s) na Fatima (sa); alisomea katika shule ya ubinadamu na utumishi, na kando ya Hassan na Hussain (a.s), alifahamu njia ya uhuru. Yeye, ambaye hakuwa nabii wala wasii, lakini katika zama za upweke wa wilaya, alirithi ujumbe wa risala, na pale kambi ya Ashura ilipofika kwenye uwanja wa majaribu, yeye pia alikuwa pale; akiwa na mwili uliokatazwa na moyo wenye uvumba wa bahari. Pia alijitolea, lakini si kwa upanga; bali kwa kamba za utumwa, kwa kuangalia maiti, kwa moto wa hema, na kwa kuona upweke wa mioyo ya watoto wadogo.
Na bibi Zainabu (sa), alitimiza mfano kamili wa aya hii: «وَبَشِّرِ الصَّابِرِینَ» (Na uwabashirie wenye kusubiri):
Yeye aliyevumilia jaribu kubwa la Karbala, si kwa hisia za upweke bali kwa imani thabiti. Wakati Ibn Ziyad kwa aibu aliuliza: “Ulikuwa unaona Mungu alifanya nini kwa ndugu yako?”
Jibu lake halikutoka kwenye moyo wa jiwe, bali kutoka katika moyo ulioona uzuri wa Mwenyezi Mungu katika vita vya damu vya Ashura.
Bibi Zainabu (sa) alikuwa miongoni mwa waliothabiti waliokuwa nyuma ya shahada ya Hussain (a.s), hakukimbia, bali alibaki, alisimama, aliongea, alifunua, na bendera ya ukweli iliyotapakaa damu iliifikisha kwa maneno.
katika mji wa Kufa, mjini Sham na mbele ya viti vya dhuluma za dhahabu, yeye ndiye aliyevunja minara ya majumba na kubana pumzi ya Yazid. Yeye ndiye aliyefanya Khutba yake kuifanya Karbala kuwa ya milele. Yeye ndiye ambaye kama asingekuwepo, Ashura ingesalia kuwa siku ya Ashura tu, lakini yeye aliifanya Ashura kuwa shule ya uamsho katika historia yote.
Na uvumilivu ni sharti la kuongoka, na bibi Zainabu (sa) alikuwa taa ya mwongozo kwa maana alitafsiri maana ya uvumilivu.
Zainabu Kubra (sa) siyo tu mfano wa mwanamke Muislamu, bali ni dhihirisho la mapenzi ya Mungu mbele ya dhulma, Yeye ni mfano wa mwanamke ambaye katengeneza mbegu za ufahamu katikati ya taabu, na kwa msimamo thabiti anaendeleza njia ya manabii.
Na leo, kila mwanamke anayetaka kuendeleza njia ya bibi Fatima (sa) na kuwa sauti ya Hussain (a.s), lazima atoke katika shule ya bibi Zainabu (sa), kwa sababu ujumbe wa Ashura bado uko mabegani mwa bibi Zainabu.
Zainabu (sa) hakuwa tu "kipambo cha baba"; yeye alikuwa kipambo cha ukweli na mwakilishi wa uvumilivu wa Ali, ufahamu wa Nabii, na heshima ya Fatima.
Maoni yako