Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Nouri Hamedani, alipokutana na kundi la wanazuoni na walimu wa Hawza ya Qom, alisisitiza kuwa: Katika hali inayo tukabili, upande wa mabeberu umeungana, na lengo letu kuu linapaswa kuwa ni kuleta umoja na mshikamano, mifarakano ni mibaya zaidi kuliko vikwazo na vita vya adui, lengo letu sote linapaswa kuwa ni kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, tusijione sisi wenyewe kuwa wa muhimu zaidi; kwa kufanya hivyo, hakuna tatizo litakalojitokeza.”
Aliongeza kwa kusema: “Leo, jukumu letu sisi watu wa hawza, ni kuielewa hali ilivyo sasa, kuwa na maarifa ya wakati na mazingira tuliyonayo, na kazi yetu ya kwanza iwe kutatua matatizo ya wananchi, muda wa kuwa tuko pamoja na Mwenyezi Mungu, watu hawa ni lazima tuwe nao, tusizembee dhidi ya munkari, umoja katika jamii ndio utuhukumu, na kusiwe na mfarakano, na tuwe na imani na kiongozi wetu, kama tutayafanya haya, basi hakika tutazivuka changamoto hizi zote, na adui wa muda mrefu wa taifa la Iran hatapata mafanikio yeyote.”
Aliendelea kusema: Sisi wanafunzi wa hawza hatupaswi kujitenga na jamii, mimi mwenyewe kwa muda mrefu nilikuwa natoka nje, naenda kununua mahitaji yangu mwenyewe, nasafiri kwenda mikoani, na kuzungumza ana kwa ana na watu, hata sasa kwa kadri ya uwezo wangu ninajitahidi kufahamu wanayo yapitia watu wengine, kuwasaidia na kutatua matatizo yao pamoja kuwapa mazingatio yanayofaa.”
Maoni yako