Jumapili 6 Aprili 2025 - 00:19
Uchumi imara ni ule unaojengwa pamoja na ushirikiano wa wananchi

Khatibu wa Swala ya Ijumaa katika mji wa Qom (Iran) amesema: Uzalishaji ni msingi na mhimili wa uchumi salama, na akaongeza kwamba uchumi imara ni ule unao simamamia ushiriki wa wananchi, uchumi wa serikali usiohusisha wananchi hauwezi kufaulu.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza Arafi, katika khutba za Swala ya Ijumaa wiki hii, alisema: "Kiongozi mkuu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa "uwekezaji katika uzalishaji" ni miongoni mwa nguzo za uchumi wa kujitegemea na unaoendelea, na amewataka watu wote kuimarisha, kuendeleza na kupanua uzalishaji pamoja na uwekezaji."

Imamu wa Ijumaa wa Qom alisisitiza kuwa, uzalishaji ni msingi mkuu wa uchumi ulio imara, na akaendelea kusema: "Uchumi imara ni uchumi unaojengwa juu ya ushiriki wa watu, wananchi ndio msingi madhubuti wa uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi, uchumi wa serikali bila ya ushiriki wa wananchi hauwezi kufaulu, mantiki ya kiislamu pia inaegemea kwenye uchumi wa wananchi, chini ya mwongozo na msaada wa serikali na taasisi husika."

Mudiri wa Hawza zote alisisitiza umuhimu wa kutumia maarifa katika uzalishaji na uchumi, na akakumbushia: "Tunapaswa kulijenga suala la uzalishaji juu ya misingi ya kimaendeleo ya kielimu na teknolojia za kisasa."

Aliashiria umuhimu wa haki na usawa katika uchumi kwa kusema: "Shughuli za kiuchumi zinapaswa kupangwa kwa namna ambayo zinafungua milango ya maendeleo kwa vijana na wale wenye vipaji."

Khatibu wa Ijumaa wa Qom, alitaja suala la kuzingatia utamaduni kama kipengele kingine muhimu, na akasema: "Katika shughuli za kiuchumi, tunapaswa kuzingatia misingi ya kiutamaduni, kiongozi mkuu wa mapinduzi amesema kuwa: Kila hatua inahitaji kuwa na nyongeza ya kiutamaduni."

Pia alisisitiza umuhimu wa kuheshimu taratibu, mazingira, na afya ya jamii, na akasema: "Kwa sasa, suala la mazingira limekuwa ajenda ya kimataifa, maendeleo ya viwanda yameipeleka Dunia kuelekea kwenye hatari kubwa, katika kila shughuli ya uzalishaji na kiuchumi, tunapaswa kuzingatia mazingira, afya ya jamii, na kupunguza matumizi ya nishati."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha