Jumamosi 5 Aprili 2025 - 06:04
Wanamichezo wakosoa mpango wa Ufaransa kupiga marufuku Hijabu katika mashindano

Wanamichezo wanawake wa Kiislamu nchini Ufaransa wamejitokeza kupinga muswada mpya wa sheria unaolenga kupiga marufuku uvaaji wa Hijabu katika mashindano ya michezo ya kitaifa, wakisema hatua hiyo inakiuka uhuru wa dini na kujieleza.

Shirika la Habari la Hawza - Kulingana na IQNA, Sylvie Eberena, mnyanyua vyuma Mwislamu mwenye umri wa miaka 44 aliyejinyakulia ubingwa wa taifa mwaka jana, sasa anahofia kupoteza haki ya kushiriki michezo kwa sababu ya Hijabu yake. Anasema, “Kila wakati, wanazidi kupunguza uhuru wetu. Sisi tunataka tu kushiriki katika michezo.”

Kwa sasa, mashirikisho ya kitaifa ya michezo yako huru kuamua kuhusu hijabu, lakini sheria mpya inalenga kuizuia kabisa vazi hilo la staha katika mashindano yote.

Wakosoaji wa sheria hiyo wanasema inalenga moja kwa moja wanawake Waislamu wanaoonekana waziwazi kuwa waumini, huku ikikiuka misingi ya usawa na ujumuishaji.

Mwanajudo wa Olimpiki wa Ufaransa, Teddy Riner, anasema mwezi uliopita kuwa mjadala huo “unapoteza muda” na kwamba Ufaransa inapaswa kuangazia usawa badala ya kushambulia dini moja pekee.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani Bruno Retailleau mwenye misiamo mikali ya mrenfo wa kulia alidai kuwa “alama ya ukandamizaji.”

Audrey Devaux, mchezaji wa mpira wa kikapu, na Samia Bouljedri, mchezaji wa mpira wa miguu, wote wameathirika na marufuku hizo. Klabu ya Samia ilitozwa faini kwa kumruhusu kucheza akiwa na Hijabu, na hatimaye aliambiwa avue hijabu au aache kabisa.

Mtafiti Rim-Sarah Alouane amesema sheria ya mwaka 1905 iliyolenga kutenganisha dini na serikali sasa “inatumiwa kama silaha dhidi ya Waislamu.”

Mashirika ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa yametaja kanuni hizo kuwa zinabagua na si za haki.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha