Alhamisi 27 Machi 2025 - 11:15
Viongozi na Wakuu wa Kiislamu wanapaswa kusimama dhidi ya uhalifu wa Wazayuni /wito wa kushiriki kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Quds

Hadhrat Ayatollah Makarem Shirazi aliwaambia Waislamu washiriki kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Quds, aliweka wazi kuwa: Viongozi na marais wa nchi za kiislamu wanapaswa kuwa na azma thabiti na wasiwe ni wenye kupuuza uhalifu unaofanywa na Wazayuni.

Kwa mujibu wa habari kutoka Shirika la Habari la Hawza, ujumbe kamili wa Ayatollah Makarem Shirazi kwa ajili ya Siku ya Quds ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Kila mwaka, Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani ni siku ya mshikamano wa Waislamu wote na watu huru Duniani katika kutetea haki za watu wa Palestina waliokandamizwa, na kusaidia kuachiliwa kwa Msikiti wa Al-Aqsa kutoka mikononi mwa wavamizi.

Katika mwaka uliopita, ulimwengu ulishuhudia matukio ya kusikitisha na ya kuhuzunisha moyo ya mashambulizi ya kikatili yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya ukanda wa Ghaza pamoja na miji mengine na vijiji vya Palestina na Lebanon mbele ya macho ya watu Duniani, Wanawake, watoto, na wazee walilengwa na mabomu ya uzito mkubwa wakiwa majumbani mwao, wagonjwa waliteketea kwa moto wakiwa hospitalini, na vijana walishuhudiwa wakishambuliwa kwa risasi za moja kwa moja, utawala huu wa kinyama, ukisaidiwa na Marekani, haukuwa na aibu yeyote katika kufanya uhalifu dhidi ya watu wasio na hatia, na serikali za magharibi, mashirika ya kimataifa pamoja na taasisi zinazodai kutetea haki za binadamu hazikuchukua hatua yeyote muhimu kwa ajili ya kuzuia uhalifu huu.

Inshallah, waislamu wote duniani, kutokana na kushiriki kwao kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Quds,  watakuwa ni miongoni mwa wale wanaokemea uhalifu huu uanaofanywa na utawala wa kizayuni, na watawapa faraja na nguvu Mujahidina wa Palestina na Lebanon.

Viongozi na marais wa nchi za kiislamu wanapaswa kuwa na azma thabiti na kutumia kila njia na rasilimali zinazowezekana kuunga mkono wahanga wanaopitia mateso na hawapaswi kupuuzia uhalifu huu.

Namuomba Mwenyezi Mungu aupe heshima uislamu na waislamu, na kuwaangamiza maadui wa uislamu, hasa utawala wa kizayuni.

Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka

Qum - Nasser Makarem Shirazi  
25 Ramadhani 1446 H

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha